Kiungo wa kati wa Manchester United na Ureno Bruno Fernandes, 30, analengwa na Real Madrid kwa pauni milioni 90. (Star)
Mkurugenzi wa michezo wa Arsenal anayekuja, Andrea Berta atakuwa na kibarua cha kukamilisha dili la kiungo wa kati wa Real Sociedad na Uhispania Martin Zubimendi huku kukiwa na nia ya kumnunua mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 26 kutoka Real Madrid. (Mirror)
Manchester City inamtazama mchezaji wa kimataifa wa Uhispania Pedri kama chaguo bora kwa safu yao ya kiungo lakini Barcelona hawana nia ya kumuuza mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 22. (Fichajes – In Spanish)
Manchester City wamefanya mazungumzo ya mapema kuhusu kumsajili kiungo wa kati wa Sweden Hugo Larsson, 20, huku Eintracht Frankfurt wakishikilia kwa angalau pauni milioni 50. (Sky Sports Germany)