Iliripotiwa mwishoni mwa mwezi uliopita kwamba Alexander-Arnold, ambaye mkataba wake unaisha mwishoni mwa msimu, alikuwa amekubaliana na wapenzi wake wa muda mrefu Real Madrid kuondoka katika klabu yake ya utotoni na kujiunga nao.
Habari hizo zinakuja kama pigo kwa kikosi cha Slot, lakini bosi huyo amesisitiza kwamba vipaumbele vyake vinabaki katika kuiongoza timu hiyo kwenye matokeo uwanjani na kumsaidia Alexander-Arnold kupona jeraha alilopata dhidi ya Paris Saint-Germain kabla ya mapumziko ya kimataifa.
"Hali yake kwa bahati mbaya ni kwamba amejeruhiwa," Slot alisema. "Vinginevyo watu wangesema kwamba alikuwa na onyesho moja au mbili nzuri kwa timu ya England.
"Lakini amejeruhiwa na kwake hiyo inamaanisha kuwa amezingatia kikamilifu kupona kwake. Kwetu sisi inamaanisha tutajaribu kumsaidia kurudi haraka iwezekanavyo," alieleza mkufunzi huyo.
Kocha huyo pia aliongeza kwamba kumekuwepo na mambo mengi ya kuwahusu Alexander Arnold, Van Dijk na Mo Salah ila wao kama viongozi wa timu hawajazingatia sana mazungumzo hayo.
"Na kwa wengine, kwa miezi minane iliyopita kumekuwa na maneno juu na chini na mazungumzo juu ya Virgil van Dijk na Mo Salah, lakini hatujawahi kuzingatia mazungumzo hayo. Daima tumekuwa tukizingatia kile tunachopaswa kufanya," aleleza.
"Ni hali ambayo iko kwa miezi minane au tisa sasa na nadhani wachezaji hawa wote watatu wamefanya vizuri sana chini ya hali hizi kwa hivyo hainiathiri hata kidogo." aliongeza.