- Lampard aonyeshwa mlango baada ya miezi 18 usukani
- The blues hata hivyo imejipata pabaya katika ligi ya premier baada ya kushindwa katika mechi za nane zilizopita .
Chelsea imemfuta kazi kocha Frank Lampard baada ya kuwa hatamuni kwa miezi 18 .
Lampard ,mwenye umri wa miaka 42 awali alikuwa kiungo wa kati katika kilabu hiyo na anaiacha Chelsea katika nafasi ya 9 kwenye jedwali la ligi ya premia baada ya kushindwa wiki jana na Leicester City na wameshinda mchuano mmoja pekee katika mechi tano za ligi . Mchuano wake wa mwisho ulikuwa siku ya jumapili katika kombe la FA raundi ya nne ambapo waliishinda Luton mabao matatu kwa moja .
Lampard aliteuliwa kocha wa The Blues kwa mkataba wa miaka mitatu alipochukua nafasi hiyo kutoka kwa Maurizio Sarri julai mwaka wa 2019
Aliwaongoza kumaliza katika nafasi ya nne katika fainali ya kombe la FA katika kipindi chake cha kwanza usukani . The blues hata hivyo imejipata pabaya katika ligi ya premier baada ya kushindwa katika mechi za nane zilizopita .