CAF

Ahmad Ahmad arejea katika uongozi wa Caf baada ya uamuzi wa mahakama

Ikiwa Cas itamkuta na hatia katika shauri litakalosikilizwa mwezi Machi, Ahmad atatolewa nje ya kinyang'anyiro moja kwa moja.

Muhtasari
  • Cas inasema itasikiliza kwa kikamilifu  rufaa ya Ahmad tarehe 2 mwezi Machi , na uamuzi uliotolewa kabla ya uchaguzi wa urais wa Caf tarehe 12 mwezi Machi.
  • Kwa kuwa alipigwa marufuku wakati Fifa ilipokutana Jumanne na Caf siku ya Alhamisi kuwajadili wagombea wa urais, Ahmad alionekana kuwa hana haki ya kugombea.
Ahmad Ahmad

 

Ahmad Ahmad wa Madagascar amerejeshwa kuwa Rais wa Shirikisho la Soka la Afrika (Caf) baada ya uamuzi wa Mahakama ya Usuluhishi wa Michezo (Cas) kuamuru hivyo

Ahmad alipigwa marufuku na Fifa mnamo Novemba kwa miaka mitano baada ya shirikisho la mpira wa miguu kuthibitisha kukiuka kanuni kadhaa za maadili.

Raia huyo wa Madagascar - ambaye sasa ataanza tena jukumu lake kama Makamu wa Rais wa Fifa - alikata rufaa kwa mahakama ya Cas, ambayo ilitoa uamuzi wa awali siku ya Ijumaa.

Ahmad bado hana haki ya kushiriki uchaguzi wa urais wa Caf mnamo utakaofanyika mwezi Machi, kwani uamuzi wa Cas ulikuja baada ya Kamati ya Utawala ya Caf na Kamati ya Ukaguzi ya Fifa kukutana mapema wiki hii kuwajadili wagombea wa nafasi hiyo.

Cas inasema itasikiliza kwa kikamilifu  rufaa ya Ahmad tarehe 2 mwezi Machi , na uamuzi uliotolewa kabla ya uchaguzi wa urais wa Caf tarehe 12 mwezi Machi.

Kwa kuwa alipigwa marufuku wakati Fifa ilipokutana Jumanne na Caf siku ya Alhamisi kuwajadili wagombea wa urais, Ahmad alionekana kuwa hana haki ya kugombea.

Sasa atahitaji kutengua maamuzi yanayomfanya asiwe na haki ya kugombea, kwani rufaa yake huko Cas haikuwa dhidi ya uamuzi uliomzuia kushiriki uchaguzi bali dhidi ya marufuku ya Fifa.

Ikiwa Cas itamkuta na hatia katika shauri litakalosikilizwa mwezi Machi, Ahmad atatolewa nje ya kinyang'anyiro moja kwa moja.

Ikiwa atashinda rufaa dhidi ya hatua ya kutogombea urais pia adhabu ya Fifa dhidi yake , Ahmad ambaye alikuwa akitangaza kuungwa mkono na mashirikisho 46, kati ya 54, muda mfupi kabla ya marufuku dhidi yake atapata nafasi ya kurudi tena.

Kufikia wiki hii, wagombea wanne walithibitishwa kugombea uchaguzi wa Caf huko Morocco nao Jacques Anouma (Ivory Coast), Patrice Motsepe (Afrika Kusini), Augustin Senghor (Senegal), Ahmed Yahya (Mauritania).