Jose Mourinho ateuliwa kuwa meneja wa Roma

Muhtasari
  • Jose Mourinho ameteuliwa kuwa meneja wa Roma tangu mwanzo wa msimu wa 2021-22
  • Mourinho, 58 atachukua nafasi ya Mreno mwenzake Paulo Fonseca, ambaye Roma ilitangaza mapema Jumanne ataondoka mwishoni mwa msimu huu
index
index

Jose Mourinho ameteuliwa kuwa meneja wa Roma tangu mwanzo wa msimu wa 2021-22.

Mourinho, 58 atachukua nafasi ya Mreno mwenzake Paulo Fonseca, ambaye Roma ilitangaza mapema Jumanne ataondoka mwishoni mwa msimu huu.

Mourinho alifutwa kazi kama bosi wa Tottenham Hotspur mnamo Aprili 19 na alikuwa amesema "atasubiri kurudi kwenye mpira" kufuatia kufukuzwa kwake.

Amesaini mkataba wa miaka mitatu na Roma, ambao ni wa saba katika Serie A.

"Asante kwa familia ya Friedkin kwa kunichagua kuniongoza kilabu hiki kizuri na kuwa sehemu ya maono yao,

Baada ya mikutano na umiliki na Tiago Pinto, nilielewa mara moja kiwango kamili cha matamanio yao

Ni tamaa na dhamira ileile ambayo imekuwa ikinihamasisha kila wakati na kwa pamoja tunataka kujenga mradi wa kushinda.

Shauku nzuri ya mashabiki wa Roma ilinishawishi kukubali kazi hiyo na siwezi kusubiri kuanza msimu ujao." Mourinho Alisema.