Mshambuliaji Harry Kane ataka kuhamia Man City

Muhtasari

• Mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 27 anaamini kwamba ana makubaliano ya mazungumzo na mwenyekiti wa Spurs Daniel Levy kumuwacha aondoke mwisho wa msimu huu.

Image: GETTY IMAGES

Mshambuliaji wa England Harry Kane amesema anataka kuhamia Man City huku akiendelea kusukuma juhudi za kuondoka katika klabu ya Tottenham mwusho wa msimu.

Mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 27 anaamini kwamba ana makubaliano ya mazungumzo na mwenyekiti wa Spurs Daniel Levy kumuwacha aondoke mwisho wa msimu huu baada ya levy kumshawishi kusalia kwa msimu mmoja zaidi. (Times - subscription required)

Hatahivyo Man United iko tayari kumuuza mashambuliaji wa Ufaransa Anthony Martial, 25, pamoja na mshambuliaji wa England Jesse Lingard - ambaye yuko kwa mkopo katika klabu ya West Ham kama njia ya kumleta Kane katika klabu hiyo.. (Football Insider)

Image: GETTY IMAGES

Manchester United huenda ikawasilisha ombi la kumnunua mshambuliaji wa Southampton na England Danny ings ,28 , mwisho wa msimu ili kuimarisha safu ya mashambulizi ya mkufunzi Ole Gunnar Solskjaer.. (Telegraph - subscription required)

Chelsea imezindua ombi la dau la £80m kumnunua mshambuliaji wa England na Borrusia Dortmund Jadon Sancho , lakini klabu hiyo ya London inakabiliwa na ushindani mkali kutoka kwa Man United kumnyakua mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 21.. (Sun)

Baadhi ya klabu barani Ulaya , ikiwemo Tottenham , Chelsea, Borussia Dortmund na AC Milan zinatarajiwa kushindana kumsaini kipa wa England Dean Henderson, kutoka Man united. (Sky Sports)

Kiungo wa kati wa Juventus na Wales Aaron Ramsey ameivutia klabu ya Liverpool kulingana na ripoti nchini Itali . The Reds wamesemekana kufikiria kuwasilisha ombi la kumnunua mchezaji huyo wa zamani wa Arsenal katika dirisha lijalo la uhamisho.. (Tutto Juve - in Italian)

Chelsea imehusishwa na ununuzi wa kiungo wa kati wa Ufaransa na Monaco 21.. (Goal)

Mkufunzi wa Bayern anayeondoka Hansi Flick, 56, ambaye amehusishwa pakubwa na kazi ya kuifunza timu ya taifa ya Ujerumani , anatakiwa na Barcelona kama mkufunzi atakayechukua mahala pake mkufunzi aliyepo sasa Ronald Koeman . (RAC1 - in Spanish)

Image: GETTY IMAGES

Barcelona iko tayari kusikiliza ofa za mshindi wa kombe la dunia Mfaransa Antoine Griezman ili kupunguza mzigo wa kifedha wa klabu hiyo. (Marca)

Griezmann, 30, huenda akarudi katika kkabu yake ya zamani ya Atletico Madrid katika makubaliano ambayo huenda yakampatia fursa Joao Felix kuelekea Barcelona , ijapokuwa klabu hiyo ya Catalan haijakubali ofa hiyo.. (Sport - in Spanish)

Klabu ya Jose Mourinho , Roma ipo katika nafasi nzuri ya kumsaini mshambuliaji wa Itali na Torino Andrea Belotti. AC Milan pia wapo mbioni kutaka kumsaini mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 27 , lakini pia wanamlenga mashambuliaji wa Chelsea na Ufaransa Olivier Giroud, ambaye kandarasi yake inakamilika mwisho mwa msimu huu. (Calcio Mercato - in Italian)

Image: GETTY IMAGES

Everton na Arsenal wanamchunguza beki wa Real Betis Emerson Royal. Mchezaji huyo wa Brazil , 22, yupo kwa mkopo kutoka Barcelona lakini huenda akavutiwa kucheza katika ligi ya Premia iwapo hatochezeshwa mara kwa mara katika uwanja wa Nou. (Sport - in Spanish)