(+PICHA)Mchezaji wa zamani wa Harambee Stars mwendazake Zablon Amanaka azikwa

Muhtasari
  • Mchezaji wa zamani wa Harambee Stars Zablon Amanaka azikwa
  • Kulingana na upasuaji wa mwili Zablon aliaga kutokana na ugonjwa wa moyo
Image: Martin Ombima

Hafla ya mazishi ya Mchezaji wa zamani wa timu ya kandanda ya Harambee Stars Zablon Amanaka inaendelea.

Mchezaji huyo aliaga dunia mnamo tarehe 28 Mei 2021, alipatikana nyumbani kwake akiwa amekata roho.

Kulingana na upasuaji wa mwili Zablon aliaga kutokana na ugonjwa wa moyo.

Zablon Amanaka ni mchezaji wa zamani wa Harambee stars, pia aliichezea Tusker AFC Leopard Sofapaka Thika united kati ya vilabu vingine.

Kutoka kwetu wanajambo Mungu ailaze roho yake mahali Pema peponi.

Hizi hapa baadhi ya picha za hafla hiyo;

Image: Martin Ombima
Image: Martin Ombima
Image: Martin Ombima
Image: Martin Ombima