HONGERA OKUMU

Mlinzi wa Harambee Stars, Joseph Okumu asajiliwa na KAA Gent ya Ubelgiji

Okumu, 24, ambaye anavaa jezi nambari 2 ya timu ya taifa ametia saini mkataba wa miaka tano na mabingwa hao wa ligi ya Ubelgiji msimu wa 2014/15.

Muhtasari

•Mlinzi huyo alianza taaluma yake ya kucheza kandanda na klabu ya Chemelil Sugar mwaka wa 2014 kabla ya kusajili na klabu ya Afrika Kusini Free State Stars mwaka wa 2016.

• Okumu amekuwa akihusishwa kwenye mechi za timu ya taifa Harambee Stars kutokana na ubora wake.

Joseph Okumu
Joseph Okumu
Image: Hisani

Mlinzi matata wa timu ya Harambee Stars. Joseph Okumu amesajiliwa katika klabu ya KAA Gent nchini Ubelgiji.

Okumu, 24, ambaye anavaa jezi nambari 2 ya timu ya taifa ametia saini  mkataba wa miaka minne na mabingwa hao wa ligi ya Ubelgiji msimu wa 2014/15.

Mlinzi huyo alianza taaluma yake ya kucheza kandanda na klabu ya Chemelil Sugar mwaka wa 2014 kabla ya kusajili na klabu ya Afrika Kusini Free State Stars mwaka wa 2016.

Baadae alichezea klabu ya AFC Ann Arbor na Real Monarchs zilizo Marekani na hivi karibuni  IF Elfsborg ya Uswidi.

Meneja wa klabu ya Gent, Tim Matthys amemsifia Okumu kama mlinzi bora.

"Joseph ni mlinzi wa kati mzuri sana na ataongeza talanta kubwa kwenye safu yetu ya ulinzi. Anapitisha mpira vizuri sana na anajiamini, ndio maana klabu nyingi zimemtamani. Tuna raha kuwa ametuchagua" Matthys alisema.

Okumu amekuwa akihusishwa kwenye mechi za timu ya taifa Harambee Stars kutokana na ubora wake.