KIPINDI CHA UHAMISHO 2021

Lionel Messi ni mchezaji huru- je anaelekea wapi?

Kwa sasa anapatikana bila gharama yoyote.

Muhtasari

•Kandarasi ya nyota huyo wa Argentina ilikamilika usiku wa kuamkia Alhamisi na licha ya miezi kadhaa ya uvumi amekataa kuongeza kandarasi yake.

•Messi anajua kwamba klabu kadhaa zinamuwania , lakini hadi kufikia sasa hajaafikia makubaliano yoyote navyo, akisubiri kusikia ofa ya Barcelona.

Lionel Messi
Lionel Messi
Image: Getty Images

Mmoja ya wachezaji maarufu zaidi wa kandanda duniani sasa ni mchezaji huru.

Ndio ,miezi 12 tangu jaribio lake la kutaka kuondoka Barcelona kutibuka , Lionel sasa ni mchezaji huru baada ya kandarasi yake kukamilika.

Kandarasi ya nyota huyo wa Argentina ilikamilika usiku wa kuamkia Alhamisi na licha ya miezi kadhaa ya uvumi amekataa kuongeza kandarasi yake.

Mazungumzo kuhusu kandarasi mpya yanaaminika kuendelea, ikimaanisha kwamba Messi huenda akaamua kusalia Nou Camp.

Lakini kwa sasa anapatikana bila gharama yoyote.

Je Messi ataelekea wapi?

Mwandishi wa soka wa Uhispania Guillem Balague alisema mapema wiki hii kwamba Barcelona imeanzisha mazungumzo ya dharura, ikiwa na matumaini ya kutangaza kandarasi mpya ya miaka miwili kabla ya mwanzo wa mwezi Julai.

Kandarasi ya Messi ndio jukumu kubwa la rais mpya wa Barcelona Joan Laporta na kwasasa anajadiliana moja kwa moja na babake Messi na mwakilishi wake Jorge Messi, alisema.

Ili kuweza kumzuia raia huyo wa Argentina kutoondoka klabu hiyo italazimika kupunguza matumizi yake kwa Yuro milioni 200 ili kumpata Messi ili kuafikia masharti ya kifedha ya 'fair Play'.

Messi anajua kwamba klabu kadhaa zinamuwania , lakini hadi kufikia sasa hajaafikia makubaliano yoyote navyo, akisubiri kusikia ofa ya Barcelona.

Mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 34 amehusishwa na uhamisho wa kuelekea PSG na Manchester City, ambapo atakutanishwa tena na mkufunzi wake wa zamani Pep Guardiola pamoja na katika ligi kuu ya Marekani.

Kwa sasa yuko mjini Barcelona akiichezea Argentina katika michuano ya Copa America na alikuwa mchezaji ambaye ameichezea nchi yake mara nyingi zaidi alipoiwakilisha kwa mara ya 148 dhidi ya Bolivia siku ya Jumanne , akiifungia mara mbili na kusaidia katika ushindi wa magoli 4-1.