EURO 2020: Italia yakatiza matumaini ya Uingereza kumaliza ukame wa miaka 55

England ilikosa kufunga mikwaju mitatu ya penalti kati ya mitano waliopewa huku wachezaji Marcus Rashford ,Jadon Sancho na Bukayo Saka wakikosa kufunga

Muhtasari

•Baada ya kipindi kigumu cha muda wa ziada ,mshindi hakupatikana timu hzo zilipotoka sare ya bao moja na ikalazimu mikwaju ya penalti kutumiwa kumpata mshindi .Huo ndio uliokuwa mwanzo wa mafadhaiko ya kocha Gareth Southgate na wachezaji wake walioingia fainali kwa matumaini makubwa .

•The three Lions , walishiriki kwenye fainali yao ya kwanza kwa wanaume kwa miaka 55, na walishindwa kupitia penalti kufuatia ya sare 1-1 baada ya dakika 120.

Washindi wa EURO 2020, Italia
Washindi wa EURO 2020, Italia
Image: TWITTER

Matumaini ya kumaliza ukame wa miaka 55 bila taji kubwa yalivunjwa jana kwa kushindwa na Italia kupitia mikwaju ya Penalti na kuipa Italia ushindi wa kombe la Euro 2020 uwanjani Wembley

Italy, ambao hawajashindwa katika mechi 33 kabla ya fainali walijirejesh polepole mchezoni na wakasawazisha katika dakika ya 67 baada ya England kutangulia kufung mapema katika kipindi cha kwanza .

Baada ya kipindi kigumu cha muda wa ziada ,mshindi hakupatikana timu hzo zilipotoka sare ya bao moja na ikalazimu mikwaju ya penalti kutumiwa kumpata mshindi .Huo ndio uliokuwa mwanzo wa mafadhaiko ya kocha Gareth Southgate na wachezaji wake walioingia fainali kwa matumaini makubwa .

England ilikosa kufunga mikwaju mitatu ya penalti kati ya mitano waliopewa huku wachezaji Marcus Rashford ,Jadon Sancho na Bukayo Saka wakikosa kufunga

Harry Kane na Harry Maguire waliifungia England ilhali Pickford mikwaju ya Andrea Belotti na Jorginho ilhali Domenico Berardi, Bonucci na Federico Bernardeschi waliifungia Italia.

Kushindwa kwa England kwa Euro 2020 na Italia ni "chungu mno" lakini wachezaji walijitolea kwa hali na mali', alisema meneja Gareth Southgate.

The three Lions , walishiriki kwenye fainali yao ya kwanza kwa wanaume kwa miaka 55, na walishindwa kupitia penalti kufuatia ya sare 1-1 baada ya dakika 120.

"Sisi sote tuko pamoja. Wameipa nchi kumbukumbu zisizoweza kuaminika," Southgate alisema kwenye BBC One.

Nahodha Harry Kane alisema kushindwa huko "kutaumiza muda uliosalia wa taaluma zetu ".

Safari za timu hizi kuingia fainali

Italia ilianza safari ya kufika fainali ya mwaka huu ya Euro kwa kushinda mechi zake zote za kundi A kwa kuichapa Uturuki 3-0, ikailaza Switzerland 3-0 kabla ya kuilaza Wales 1-0. Hatua ya 16 bora ikaichapa Austria 2-1, ikakutana robo fainali na Ubelgiji ikawalaza 2-1 kabla ya kuiondosha kwa matuta 4-2 Hispania baada ya dakika 120 kumalizika kwa sare ya 1-1.

Timu ya taifa ya Uingereza
Timu ya taifa ya Uingereza

England iliyowaondoa Denmark katika nusu fainali kwa kuichabanga 2-1, ilianza safari yake kwa ushindi wa bao 1-0 dhidi ya Croatia, ikaenda sare tasa ya 0-0 na ndugu zao wa Scotland kabla ya kumaliza michezo yake ya kundi D kwa ushindi wa bao 1-0 dhidi ya Czech Republic. 16 bora ilikutana na Ujerumani ikapata ushindi wa kihistoria wa mabao 2-0 kabla ya kuiondosha Ukraine kwenye robo fainali kwa kapu la mabao 4-0