FKF yasimamisha kazi maafisa 5 wa FKF-PL waliokabiliwa na tuhuma za udanganyifu kwenye mechi

FKF kwa ushirikiano na FIFA wameanza uchunguzi kubaini iwapo ni kweli watano hao walihusika kwenye udanganyifu wa mechi zilizotajwa

Muhtasari

•Watano hao ikiwemo refa wa FIFA Raymond Onyango wamesimamishwa kazi ili kupatia nafasi uchunguzi kuendelea kufuatia tuhuma za udanganyifu kwenye mechi za kandanda nchini.

•Wengine waliosimamishwa kazi ni pamoja na Samuel Mwaura, Isaac Memusi, Collins  Opiyo na Japeth Juma.

Image: TWITTER//FKF

Shirikisho la soka nchini, FKF, limesimamisha kazi maafisa watano wanaosimamia michuano ya ligi ya soka nchini, FKF-PL.

Watano hao ikiwemo refa wa FIFA Raymond Onyango wamesimamishwa kazi ili kupatia nafasi uchunguzi kuendelea kufuatia tuhuma za udanganyifu kwenye mechi za kandanda nchini.

Wengine waliosimamishwa kazi ni pamoja na Samuel Mwaura, Isaac Memusi, Collins  Opiyo na Japeth Juma.

FKF kwa ushirikiano na FIFA wameanza uchunguzi kubaini iwapo ni kweli watano hao walihusika kwenye udanganyifu wa mechi zilizotajwa.

FKF imesema kuwa imesimamisha kazi watano hao kama tahadhari.