Gor Mahia yatangaza usajili wa kocha mpya

Kocha Harrison ambaye ana umri wa miaka 60 aliwahi chezea klabu tajika Uingereza kama Southampton, Stoke City na Port Vale.

Muhtasari

•Klabu ya Gor Mahia imetangaza kocha wake mpya wiki tatu tu baada ya kujiuzulu kwa aliyeshikilia wadhfa huyo Manuel Pinto kutoka Ureno.

•Siku za uchezaji wake, Harrison alicheza katika nafasi ya mlinda lango.

Kocha Mark Harrison azinduliwa
Kocha Mark Harrison azinduliwa
Image: TWITTER//GOR MAHIA

Klabu ya Gor Mahia imetangaza kocha wake mpya wiki tatu tu baada ya kujiuzulu kwa aliyeshikilia wadhfa huyo Manuel Pinto kutoka Ureno.

K'Ogallo ilitangaza uteuzi wa Mark Harrison kutoka Uingereza  kama kocha mpya Jumatatu jioni.

Meneja huyo mzaliwa wa Uingereza atakuwa na jukumu kubwa kujaribu kurejesha ubora wa mabingwa hao msimu uliopitia ambao hivi karibuni wamekuwa wakiandikisha matokeo hafifu.

Kocha Harrison ambaye ana umri wa miaka 60 aliwahi chezea klabu tajika Uingereza kama Southampton, Stoke City na Port Vale.

Siku za uchezaji wake, Harrison alicheza katika nafasi ya mlinda lango. Amekuwa kwenye taaluma ya kufunza na kusimamia klabu za kandanda kwa miaka zaidi  20.