Hatimaye ligi kuu Uingereza kuanza leo; Fahamu klabu ipi itacheza na nani, saa ngapi wikendi hii

Msimu wa 2021/22 unatazamiwa kuchukua miezi tisa huku mechi ya mwisho ikitarajiwa kuchezwa tarehe 22 mwezi Mei mwaka ujao.

Muhtasari

•Msimu wa 2021/22 unaanza na mechi ya kusisimua kati ya Arsenal na klabu ya Brenford iliyopandishwa ngazi msimu huu baada ya kuibuka wa tatu kwenye ligi ya Championship msimu uliopita.

•Siku ya Jumapili Newcastle itakaribisha klabu ya Westham mida ya saa kumi alasiri huku mabingwa wa ligi msimu uliopita Manchester City wakitembelea Tottenham ugani Tottenham Hotspur Stadium saa kumi na mbili unusu masaa ya Afrika Mashariki.

Image: EPL

Hatimaye ligi kuu ya Uingereza inang'oa nanga leo (Agosti 13) baada ya kuwa katika kipindi cha mapumziko kufuatia kukamilika kwa msimu wa 2020/21 mwezi Mei.

Msimu wa 2021/22 unaanza na mechi ya kusisimua kati ya Arsenal na klabu ya Brenford iliyopandishwa ngazi msimu huu baada ya kuibuka wa tatu kwenye ligi ya Championship msimu uliopita.

Mechi hiyo ya ufunguzi wa ligi itachezewa ugani Brentford Community Stadium jijini London mida ya saa nne usiku wa Ijumaa.

Siku ya Jumamosi itashuhudia mechi sita zikichezwa mechi ya kwanza ikiwa kati ya aliyeibuka wa tatu msimu uliopita, Manchester United na klabu ya Leeds United. Mechi hiyo itachezwa mida ya saa nane alasiri.

Washindi wa lgi ya mabingwa msimu uliopita, Chelsea watamenyana na  klabu ya Crystal Palace mida ya saa kumi na moja jioni.

Mechi zingine ambazo zitakuwa zinaendelea kwa wakati huo huo ni kati ya Leicester na Wolves, Watford dhidi ya Aston Villa, Everton dhidi ya Southampton na Burnley dhidi ya Brighton.

Mechi ya mwisho siku ya Jumamosi itakuwa kati ya washindi wa ligi msimu wa 2019/20 Liverpool na klabu ya Westham. Mchuano huo utachezwa saa moja unusu jioni.

Mechi mbili pekee zitachezwa siku ya Jumapili. 

Newcastle itakaribisha klabu ya Westham mida ya saa kumi alasiri huku mabingwa wa ligi msimu uliopita Manchester City wakitembelea Tottenham ugani Tottenham Hotspur Stadium saa kumi na mbili unusu masaa ya Afrika Mashariki.

Msimu wa 2021/22 unatazamiwa kuchukua miezi tisa huku mechi ya mwisho ikitarajiwa kuchezwa tarehe 22 mwezi Mei mwaka ujao.