Mshambulizi Tammy Abraham akamilisha uhamisho kutoka Chelsea kujiunga na AS Roma

Abraham ambaye amegharimu Roma pauni milioni 34 ametia saini mkataba wa miaka mitano na atavalia jezi nambari tisa.

Muhtasari

โ€ขAbraham, 23, amejiunga na miamba hao wa Italia wanaoongozwa na kocha Jose Mourinho baada ya kuwa na 'The Blues' tangu akiwa na umri wa miaka saba.

Image: AS ROMA

Mshambulizi Tammy Abraham amemaliza uhamisho wale kutoka Chelsea na kujiunga na klabu ya AS Roma..

Abraham, 23, amejiunga na miamba hao wa Italia wanaoongozwa na kocha Jose Mourinho baada ya kuwa na 'The Blues' tangu akiwa na umri wa miaka saba.

Raia huyo wa Uingereza amefungia washindi wa ligi ya mabingwa msimu uliopita mabao 30 katika mechi 82 ambazo amecheza katika kiwango cha juu.

Abraham ambaye amegharimu Roma pauni milioni 34 ametia saini mkataba wa miaka mitano na atavalia jezi nambari tisa.

Alipokuwa anakamilisha uhamisho huo, Abraham amesema kuwa anatazamia kutumia uzoefu wake kusaidia vijana wa Mourinho kushinda mataji.

"Roma ni klabu ambayo inastahili kuwa inashindania mataji na vikombe. Niko na uzoefu wa kushinda vikombe na nataka kuwa kwa mashindano hayo tena. Natak kusaidia timu hii kuweza hayo na kufikia mahali inastahili kuwa" Abraham alisema.

Roma na Chelsea wametangaza habari kuhusu uhamisho huo kupitia tovuti rasmi za klabu hizo.

Haya yanajiri siku chache tu baada ya Chelsea kumsajili tena mshambulizi matata Romelu Lukaku kutoka klabu ya Inter Milan.