Fahamu kwa nini klabu ya Juventus inamuuza Christiano Ronaldo

Ronaldo, 36, anajulikana kughadhabishwa na jinsi uhamisho wake kwenda Juventus ulivyobadilika.

Muhtasari

•Yeye ni mmoja wa wachezaji bora wakati wote, lakini akiwa amesalia na mwaka mmoja katika mkataba wake, Juventus wako tayari kumuuza Cristiano Ronaldo

Image: GETTY IMAGES

Yeye ni mmoja wa wachezaji bora wakati wote, lakini akiwa amesalia na mwaka mmoja katika mkataba wake, Juventus wako tayari kumuuza Cristiano Ronaldo.

Timu ya wataalam wa Uropa ya Redio 5 Live - Raphael Honigstein, Julien Laurens na Kristof Terreur - wamekuwa wakijadili swali hili na zaidi:

Kwa nini Juventus wanataka kumwondoa Ronaldo?

Image: GETTY IMAGES

Ronaldo, 36, anajulikana kughadhabishwa na jinsi uhamisho wake kwenda Juventus ulivyobadilika.

Miamba hao wa Italia hawajafika robo fainali ya Ligi ya Mabingwa tangu kuwasili kwake Turin na kilabu cha Serie A kimeshindwa katika hatua ya 16 bora katika kampeni mbili zilizopita.

Msimu uliopita, walipoteza taji lao la ligi baada ya kushinda kwa miaka tisa mfululizo na kuingia tu kwenye nafasi za Ligi ya Mabingwa katika michezo michache iliyopita.

Ronaldo aliachwa nje na mkufunzi Massimiliano Allegri wakati Juventus ikitoka sare kwenye Serie A katika mechi yao ya ufunguzi dhidi ya Udinese - kitu ambacho kilabu kilisisitiza ni uamuzi wa pamoja na mchezaji huyo.

Honigstein: "Juventus wanajitahidi kumuuza Ronaldo na hata kuna mazungumzo juu yake labda aende kwa uhamisho wa bila malipo kwasababu wana hamu kubwa ya kumwondoa kwenye mshahara huku kifikra zao wakiangazia mchango wake mdogo katika timu - kwamba hautoshi.

"Aliulizwa James Horncastle ikiwa Juventus wana nguvu na Ronaldo au bila Ronaldo kwenye Ligi ya Mabingwa na hakusita kusema "bila Ronaldo".

Hivyo ndivyo Juventus inavyofikiria juu yake kwa sasa na sio kwasababu za kifedha tu.