Messi anyamazishwa katika mechi yake ya kwanza akiichezea PSG

Muhtasari

•Messi aligonga mwamba wa goli na baadaye akashindwa kuonesha umahiri wake katika mechi yake ya kwanza na badala yake ilikuwa Anders Herrera aliyefunga goli la kwanza baada ya kazi nzuri ya Mbappe upande wa kushoto.

Image: BBC

Jukumu la Lionel Messi katika klabu ya PSG litakuwa kuisaidia timu hiyo kushinda taji la klabu bingwa Ulaya , lakini licha ya sifa zote za mchezaji huyo wa Argentina , mechi yake ya kwanza akiichezea miamba hiyo ya Ufaransa ili kupanda mlima na sio kama alivyotarajia huku klabu hiyo ikianza kampeni yake kwa kupata sare dhidi ya Club Brugges.

Messi aligonga mwamba wa goli na baadaye akashindwa kuonesha umahiri wake katika mechi yake ya kwanza na badala yake ilikuwa Anders Herrera aliyefunga goli la kwanza baada ya kazi nzuri ya Mbappe upande wa kushoto.

Hans Vanaken alikomboa kwa upande wa Club Bruges kabla ya muda wa mapumziko mbele ya uwanja wa Jay Breydel uliokuwa na mashabiki 29,000.

Messi alipatiwa kadi ya njano katika kipindi cha pili na Mbappe akatolewa baada ya dakika 51 huku PSG ikishindwa kuona lango la timu ya nyumbani , ambayo inahisi kwamba ilikuwa na kila uwezo kuibuka washindi katika mechi hiyo.

PSG ilishindwa kukabiliana na timu hiyo ya nyumbani ambayo iliwazuia wachezaji wake katika kipindi chote cha mchezo huku kipa Keylor Navas akihitajika kupangua shambulio la Ketelaere ili kupata sare hiyo.