Uteuzi wa kocha mpya wa timu ya soka ya Harambee Stars wazua gumzo mitandaoni

Muhtasari

•Wakenya wamekuwa wakitumia mitandao wa kijamii ya Twitter kuelezea kutoridhishwa kwao na uteuzi wa mkufunzi mpya wa timu ya taifa ya soka Harambe stars Mturuki Engin Farat.

•Baadhi ya Wakenya wameeleza wasiwasi wao kuhusiana na matokeo hafifu ambayo kocha Firat ameandikisha na timu ambazo amekuwa akisimamia hapo awali

Engin Firat
Engin Firat
Image: FKF

Uteuzi wa kocha mpya wa timu ya taifa ya soka Kenya umezua gumzo mitandaoni.

Wakenya wamekuwa wakitumia mitandao wa kijamii ya Twitter kuelezea kutoridhishwa kwao na uteuzi wa mkufunzi mpya wa timu ya taifa ya soka Harambe stars Mturuki Engin Farat.

Shirikisho la Soka la nchini Kenya (FKF) lilitangaza uteuzi wake Siku ya Jumapili kwa kandarasi ya miezi miwili.

Baadhi ya wakenya wamekuwa wakihoji jinsi Mkuu wa FKF Nick Mwendwa alivyoafikia uteuzi huo.

Baadhi yao wameeleza wasiwasi wao kuhusiana na matokeo hafifu ambayo kocha Firat ameandikisha na timu ambazo amekuwa akisimamia hapo awali

Firat anachukua nafasi ya Jacob 'Ghost' Mulee ambaye alijiuzulu wadhifa huo siku chache zilizopita.

Mtumiaji mwingine wa mtandao huo JG anamtetea Nick Mwendwa akisema amejitahidi kadri ya uwezo wake kutatua matatizo ambayi yamekua yakiikabili Harambee Stars kwa miaka kadhaa.