Ratiba ya wiki ya sita ya EPL; Mechi za kuangaziwa zaidi

Muhtasari

•Wikendi hii itaanza kwa mechi kubwa kati ya viongozi wa ligi kwa wakati huu Chelsea na washindi wa taji la EPL 2020 Manchester City.

•Wanabunduki wanatazamia kuwanyamazisha majirani wao ambao kwa sasa wako na alama tatu juu yake. katika mchuano huo wa 'North London Derby' 

Image: HISANI

Mashindano ya ligi kuu Uingereza (EPL)  yanaingia katika wiki ya sita huku mechi 10 zikitarajiwa kuchezwa wikendi hii.

Wikendi hii itaanza kwa mechi kubwa kati ya viongozi wa ligi kwa wakati huu Chelsea na washindi wa taji la EPL 2020 Manchester City. Mechi hiyo itachezewa ugani Stamford Bridge mida ya saa nane unusu alasiri ya Jumamosi.

Chelsea watazikosa huduma za kiungo matata Mason Mount na mshambulizi Christian Pulisic ambao wanauguza majeraha huku City huenda wakakosa huduma za Ikay Gundogan, Rodri, John Stones, Oleksandr Zichenko na Aymeric Laporte ambao hali yao haijulikani kabisa baada ya kuugua majeraha.

Mechi nyingine ambayo itakuwa inaendelea kwa wakati huo ni kati ya Manchester United na Astob Villa. Manchester wanatazamia kuendelea msururu wa matokeo bora kwenye ligi huku wakikaribisha Villa ugani Old Trafford.

Mechi nne zitachezwa mida ya kumii na moja.

Everton watakaribisha Norwich ugani Goodison Park , West Ham watembelee Leeds ugani Elland Road, Leicester wakaribishe Burnley King Power Stadium na huku Newcastle wakiwa wageni wa Watford.

Mechi ya mwisho siku ya Jumamosi itachezwa saa moja unusu ambapo Liverpool watacheza dhidi ya Brentford ugenini.

Michuano miwili itapigwa siku ya Jumapili ambapo Southampton wataalika Wolves ugani St Mary's mida ya saa kumi.

Mechi nyingine ambayo inasubiriwa kwa hamu ni kati ya Arsenal na Tottenham ambao watamenyana saa moja unusu ugani Emirates.

Wanabunduki wanatazamia kuwanyamazisha majirani wao ambao kwa sasa wako na alama tatu juu yake. katika mchuano huo wa 'North London Derby' 

Mechi ya mwisho kati ya Crystal Palace na Brighton mida ya saa nne usiku wa Jumatatu.