EPL 2021/22: Matokeo ya wiki ya 6, Hali ilivyo kwenye jedwali

Muhtasari

•Kortney Hause alisaidia Villa kupata ushindi dhidi ya mashetani wekundu baada ya kufunga bao katika dakika ya 88 huku kiungo Bruno Fernandes akikosa kutia mkwanju wa penalti wavuni katika dakika za ziada na kunyima timu yake angalau pointi moja.

•Vijana wa Mikel Arteta waling'aa nyumbani huku wakifunga maadui wao wa jadi mabao matatu katika kipindi cha kwanza na kufungwa bao moja tu katika kipindi cha pili.

•Kwa sasa Liverpool, City, Chelsea na United wamekalia nafasi nne bora na pointi 14, 13, 13, 13 mtawalia huku Leeds, Burnley na Norwich wakifunga mkia na pointi 3, 2, 0 mtawalia.

Image: TWITTER// ARSENAL

Matokeo ya kushangaza mno na yasiyotarajiwa yalishuhudiwa katika Wiki ya sita ya ligi kuu Uingereza (EPL) .

Mechi za kwanza zilichezwa mida ya saa nane unusu siku ya Jumatatu ambapo Chelsea walimenyana na Manchester City ugani Stamford Bridge huku Manchester United wakikaribisha Aston Villa ugani Old Trafford.

Timu za nyumbani zilipoteza 1-0 kila mmoja dhidi ya wageni wao na kukosa nafasi za kusonga kileleni mwa jedwali la EPL 2021/22.

Mshambulizi Gabriel Jesus alifungia City bao la pekee na kusaidia washindi wa EPL 2020 kuadhibu washindi wa ligi ya mabingwa (UCL) msimu uliopita.

Kortney Hause alisaidia Villa kupata ushindi dhidi ya mashetani wekundu baada ya kufunga bao katika dakika ya 88 huku kiungo Bruno Fernandes akikosa kutia mkwanju wa penalti wavuni katika dakika za ziada na kunyima timu yake angalau pointi moja.

Mechi nne zaidi zilichezwa mida ya saa kumi na moja jioni ambapo Everton walishinda Norwich 2-0 ugani Goodison Park, West Ham wakashinda 2-1 ugenini dhidi ya Leeds, Leicester wakatoka sare ya 2-2 dhidi ya Burnley huku mechi kati ya Watford na Newcastle ikiishia sare ya 1-1.

Mchuano wa mwisho siku ya Jumamosi ulikuwa kati ya wageni kwenye ligi Brentford na washindi wa EPL 2019 Liverpool ambayo iliishia sare ya 3-3.

Mechi mbili zilichezwa siku ya Jumapili ya kwanza ikiwa kati ya Southampton  na Wolves ambayo ilichezwa ssaa kumi alasiri. Southampton walishindwa kudhibiti Wolves nyumbani na kupoteza 0-1.

Mechi ya kusisimua zaidi ilikuwa kati ya mafahari wawili wa jiji la London Arsenal na Chelsea ambayo ilichezwa mida ya saa kumi na moja unusu.

Vijana wa Mikel Arteta waling'aa nyumbani huku wakifunga maadui wao wa jadi mabao matatu katika kipindi cha kwanza na kufungwa bao moja tu katika kipindi cha pili.

Emile Smith Rowe, Pierre Emerick Aubameyang na Bukayo Saka walifungia wanabunduki huku Son Heung-Min akifungia Spurs bao moja la kufutia machozi.

Kwa sasa Liverpool, City, Chelsea na United wamekalia nafasi nne bora na pointi 14, 13, 13, 13 mtawalia huku Leeds, Burnley na Norwich wakifunga mkia na pointi 3, 2, 0 mtawalia.