Champions League 2021/22: Matokeo ya mechi za pili katika kundi A, B, C, D

Michuano ambayo ilichezwa ilihusisha klabu 16 zilizo kwenye kundi A, B, C na D.

Muhtasari

•Nyota wa soka Lionel Messi na kiungo Idrissa Gueye walisaidai vijana wa Mauricio Pochettino kupata ushindi wa 2-0 dhidi ya wageni wao City.

•Mwendo wa saa nne usiku Bayern Munich watamenyana na Dynamo Kie, Manchester United watapambana na Villareal, Juventus wapimane nguvu na Chelsea, Barcelona wacheze dhidi ya Benfica,Salzburg wapatane na Lille na Wolfsburg wacheze dhidi ya Sevilla.

Image: HISANI

Mashindano ya Champions League yaliingia katika wiki ya pili huku jumla ya mechi nane zikichezwa usiku wa Jumanne.

Michuano ambayo ilichezwa ilihusisha klabu 16 zilizo kwenye kundi A, B, C na D.

Mechi za kwanza zilichezwa mida ya saa mbili kasorobo ambapo Ajax walilaza Besiktas mabao mawili kwa sufuri wakiwa nyumbani huku mechi kati ya washindi wa Serie A msimu uliopita Juventus na Shaktar Donesk ya Ukraine ikiishia sare ya 0-0.

Mechi sita zaidi za kusisimua zilichezwa mwendo wa saa nne usiku.

Mechi ya kuangaziwa zaidi ilikuwa kati ya miamba wa soka nchini Uingereza Manchester City na wababe wa Ufaransa PSG.

Nyota wa soka Lionel Messi na kiungo Idrissa Gueye walisaidai vijana wa Mauricio Pochettino kupata ushindi wa 2-0 dhidi ya wageni wao City.

Washindi wa EPL 2019/20 Liverpool walipata ushindi mkubwa wa 5-1 ugenini dhidi ya FC Porto ya Ureno. Mohammed Salah, Sadio Mane na Roberto Firmino walifungia Liverpool huku bao la pekee la Porto likifungwa na Mehdi Taremi.

Mechi nyingine ambayo iliandikisha matokeo ya kushtukiza ni kati ya Real Madrid ya Uhispania na Sherrif Tiraspol ya Moldova ambapo vijana wa Carlo Ancelotti waliangamia kichapo cha 1-2 nyumbani.

Washindi wa Laliga msimu uliopita Atletico Madrid walipata ushindi wa 2-1 ugenini dhidi ya AC Milan ya Italia.

Mechi kati ya RB Leipzig ya Ujerumani na Club Brugge KV ya Ubelgiji iliishia 1-2 

Mechi nane zaidi zinatarajiwa kuchezwa usiku wa Jumatano huku Zenit St Petersburg wakimenyana na Malmo FF na Atlanta wakicheza dhidi ya Young Boys saa mbili kasorobo.

Mwendo wa saa nne Bayern Munich watamenyana na Dynamo Kie, Manchester United watapambana na Villareal, Juventus wapimane nguvu na Chelsea, Barcelona wacheze dhidi ya Benfica,Salzburg wapatane na Lille na Wolfsburg wacheze dhidi ya Sevilla.