Kesi ya ubakaji dhidi ya Cristiano Ronaldo lazima itupiliwe mbali - Jaji

Ronaldo amekuwa wakati wote akikana kufanya kosa lolote.

Muhtasari

•Waendesha mashitaka walichagua kutowasilisha mashitaka ya uhalifu dhidi ya Ronaldo katika mwakawa  2019 wakisema kuwa madai hayo yanaweza kuwa "hayakuthibitishwa vya kutosha".

Image: HISANI

Jaji amependekeza kuwa kesi ya ubakaji dhidi ya mshambuliaji wa Manchester United Cristiano Ronaldo nchini Marekani itupwe nje ya mahakama.

Inadaiwa kuwa Ronaldo mwenye umri wa miaka 36 alimyanyasa Kimapenzi mwanamke katika hoteli moja eneo la Las vegas mwaka 2009.

Waendesha mashitaka walichagua kutowasilisha mashitaka ya uhalifu dhidi ya Ronaldo katika mwakawa  2019 wakisema kuwa madai hayo yanaweza kuwa "hayakuthibitishwa vya kutosha".

Kesi ya kiraia ilifuatia madai ya mwanamke huyo kudai fidia ya uharibifu. Ronaldo amekuwa wakati wote akikana kufanya kosa lolote.

Hakimu Daniel Albregts, ambaye alichunguza upya kesi hiyo kabla ya jaji mwingine kufanya uamuzi wa mwisho, anasema ushahidi wenye misingi ya mawasiliano yaliyovuja baina ya Ronaldo na mawakili wake kutoka katika data zilizovuja za soka haungepaswa kutumiwa katika kesi.