Wamiliki wa Newcastle United wasihi mashabiki wasivae mavazi ya kitamaduni ya Kiarabu wakati wa mechi

Muhtasari

•Mavazi kama hayo yalionekana wakati wa mechi dhidi ya Tottenham katika mchezo wa kwanza wa kilabu chini ya wamiliki wapya.

Image: EPA

Newcastle United imewaomba mashabiki wasivae "mavazi ya kitamaduni ya Kiarabu au vazi la kufunika kichwa linalotumika Mashariki ya Kati" kwenye mechi kufuatia kununuliwa kwa kilabu hiyo na wamiliki kutoka Saudi Arabia.

Wafuasi wengine wa Magpies walivaa nguo hizo wakati walipokusanyika nje ya St James Park 'kusherehekea kununuliwa kwa kilabu hiyo

Mavazi kama hayo pia yalionekana wakati wa mechi dhidi ya Tottenham katika mchezo wa kwanza wa kilabu chini ya wamiliki wapya.

"Hakuna mtu katika kikundi kipya cha wamiliki aliyekerwa kwa njia yoyote," kilabu ilisema.

"Ilikuwa ishara ambayo ilikubaliwa kuwa nzuri na ya kukaribisha kwa nia yake.

"Walakini, kuna uwezekano wa kuwa kuvaa hivi sio sawa na kitamaduni na kuna hatari ya kukasirisha wengine.