Manchester United yaijibu Liverpool kwa kishindo

Muhtasari
  • Ole Gunnar Solskjaer amedokeza kuwa Manchester United imetoka kwenye"wiki ngumu" baada ya kupata ushindi kutoka Tottenham Nuno Espírito Santo
Image: BBC

Ole Gunnar Solskjaer amedokeza kuwa Manchester United imetoka kwenye"wiki ngumu" baada ya kupata ushindi kutoka Tottenham Nuno Espírito Santo.

Cristiano Ronaldo alikuwa nyota wa mchezo huo, ambao ulitoa jibu kamili kwa kuchapwa mabao 5-0 na Liverpool wiki iliyopita kwenye Uwanja wa Old Trafford jambo ambalo lilizua maswali mengi kuhusu mustakabali wa Solskjaer.

Solskjaer bado hajatoka kwenye wakati mgumu , lakini Ronaldo aliyafanya maisha yawe ya raha zaidi kwa bosi wake kwa kuweka mpira wavuni kutoka kwa Bruno Fernandes dakika sita kabla ya mapumziko, ikifuatiwa na pasi ambayo alimtengenezea Edinson Cavani. sekunde moja baada ya dakika 64.

"Jambo muhimu zaidi kwa mashabiki, mimi na wachezaji ni kuwa kitu kimoja," alisema bosi huyo anaye tokea nchini Norway, ambaye timu yake ilipata ushindi wa kwanza katika mechi tano za Ligi Kuu.

"Imekuwa wiki ngumu kwangu na kwa wachezaji, klabu, mashabiki. Nimekaa mbali na kelele nyingi. Lakini unajua kinachoendelea huko nje na unajua lazima uwe kwenye kiwango cha juu.

"Kila wakati unapopoteza mchezo ni hisia mbaya zaidi duniani kama kocha au meneja. Tulihitaji wiki nzima kufanyia kazi utendaji huu."

Marcus Rashford alihitimisha mambo kwa kumaliza dakika nne kabla ya mechi kumalizika huku mashabiki wa Spurs wakilipuka kwa hasira dhidi ya Nuno na mwenyekiti wao Daniel Levy, huku kelele za "tunataka Levy atoke" zikivuma kwenye uwanja huo mkubwa.

Tottenham hawakuwa na kiwango kizuri cha Harry Kane kwenye mchezo na sintofahamu miongoni mwa mashabiki wao, ambao walimgeukia meneja Nuno alipomtoa Lucas Moura na kumuingiza Steven Bergwijn katika kipindi cha pili.

Ronaldo alionyesha kipaji na uwezo wake wa hali ya juu wakati tu Solskjaer na United walivihitaji zaidi katika mchezo ambao hawakupaswa kupoteza.

Akisaidiwa na Cavani, mshambulizi huyo wa Ureno aliongezea kiwango cha hali ya juu katika mchezo wa United ambao ulikuwa uboreshaji mkubwa kutokan na matokeo yasiyo ridhisha dhidi ya Liverpool, ingawa hilo halikuwa gumu na Spurs walishindwa kuonyesha upinzani.

Ronaldo alikuwa tishio mara kwa mara na harakati zake, kwa mashambuliyo ya mara kwa mara United wakitawala.

Alionyesha ufundi mzuri kwa bao lake kisha akaonyesha muunganiko mzuri na Cavani na kumpeleka Murugwai huyo kwa umaliziaji ambao uliza goli la pili.

Solskjaer aliweza kurejesha Raphael Varane kwenye safu yake ya ulinzi pamoja na nahodha Harry Maguire na Victor Lindelof katika safu ya tatu ya nyuma ambayo ilikabiliana vyema na mashambulizi hafifu ya Spurs ya nje ya aina.

Japokuwa kwa kiwango cha Spurs kwasasa huwezi kuikiweka katika daraja sawa na Liverpool, bado ilikuwa dakika 90 za kuridhisha kwa Solskjaer baada ya wiki ya kusikitisha baada ya kupata matokeo yakusikitisha dhidi ya Liverpool mbele ya mashabiki wao.

Inaweza tu kuwa mwanzo, hata hivyo, kwa United kucheza na Atalanta nchini Italia kwenye Ligi ya Mabingwa wiki hii kabla ya kukutana na Manchester City kwenye Uwanja wa Old Trafford Jumamosi ijayo mchana.

Kuna safari ndefu kwa United na Solskjaer kutokana na kupoteza kwa Liverpool lakini palipo na Ronaldo kuna matumaini.

Meneja wa Spurs Nuno amekuwa akihangaika kupata ushindi na mashabiki lakini hali ndani ya uwanja huu mkubwa inazidi kuwa mbaya.

Tayari walikuwa katika hali mbaya kabla ya Nuno kufanya uamuzi uliokuwa na utata wa kumbadilisha Moura na kuchukua Bergwijn dakika tisa baada ya mapumziko. Uwanja huo uligubikwa na nderemo na kelele za "hujui unachofanya" zikimlenga Nuno.

Na wakati Rashford alipopita katika safu ya ulinzi na kuwaongezea jeraha, Levy alikuwa kwenye akishambuliwa na maneno huku maelfu ya mashabiki wa Spurs wakiinuka na kuondoka.

Tottenham walishindwa kulenga goli huku hata Kane akihisi kufadhaika kwa mashabiki wa nyumbani.

Hadhi ya Nuno, haiendani kabisa na orodha ya mameneja wanaotakiwa wakati Spurs ilipohamia kuchukua nafasi ya Jose Mourinho aliyetimuliwa, kila mara ilimaanisha kwamba alihitaji kuanza kwa kasi lakini mtindo wake wa kandanda la kuzuia inapelekea hasira.

Kujiamini kwa United kungekuwa hafifu baada ya matokeo dhidi ya Liverpool lakini Spurs walikuwa waangalifu sana, wakikaa na kucheza mchezo wa kusubiri ambao uliruhusu timu ya Solskjaer kuwa mchezo na kudhibiti.

Huu ulikuwa ni ubora wa pande zote na ushindi ambao ulistahiliwa kabisa

Nuno alihisi upweke kwani alihisi hasira kutoka kwa mashabiki wa Spurs, ikionekana kupotea kama ilivyokuwa kwa Solskjaer kwenye uwanja wa Old Trafford Jumapili iliyopita wakati Liverpool wakiwashushia ghasia.

Na Kane ndiye kielelezo kigumu cha maswaibu ya sasa ya Spurs, akipambana pembezoni na analengwa na mashabiki wale wale ambao walijivunia kumwita "mmoja wetu".

Kane ameonekana kuwa mchezaji tofauti, aliyepunguzwa tangu mpango wa kuhamia Manchester City ulipotimizwa msimu wa joto ingawa inapaswa kuongezwa pia kuwa huduma ya nahodha wa England ilikuwa duni.

Alikuwa Son Heung-min aliyebeba nguvu nyingi na tishio katika usiku wa taabu kabisa kwa Spurs.

Nuno sasa anahitaji ushindi haraka, na mechi ya nyumbani dhidi ya Vitesse - ambao waliifunga Spurs siku tisa zilizopita huko Arnhem - kwenye Ligi ya Mikutano ya Europa kabla ya kutembelea Everton akiwasilisha orodha ya mechi za hatari.