Karim Benzema apatikana na hatia ya ulaghai kupitia kanda ya ngono

Muhtasari

•Benzema alikuwa mmoja wa watu watano walioshtakiwa mwezi uliopita kwa jaribio la kumpunja fedha Mfaransa Mathieu Valbuena kutumia kanda hiyo.

Karim Benzema
Karim Benzema
Image: Getty Images

Mshambulizi wa timu ya taifa ya Ufaransa na Real Madrid, Karim Benzema amepatikana na hatia ya kula njama ya kumtusi mwanasoka mwenzake wa Ufaransa kutumia kanda ya ngono.

Jaji alimpa Benzema kifungo cha mwaka mmoja jela na kuamuru alipe faini ya €75,000 (£63,000; $84,000).

Benzema alikuwa mmoja wa watu watano walioshtakiwa mwezi uliopita kwa jaribio la kumpunja fedha Mfaransa Mathieu Valbuena kutumia kanda hiyo.

Kashfa hiyo imeshangaza jamii ya soka nchini Ufaransa na wachezaji wote wawili kupoteza nafasi katika timu yao ya taifa.

Kesi hiyo ilianza Juni 2015, wakati wanasoka hao wawili walikuwa kwenye kambi ya mazoezi ya Ufaransa.

Katika kambi hiyo, Benzema aliweka shinikizo kwa Valbuena kuwalipa watu waliodai kuwa na kanda hiyo, ambao alikuwa amefanya nao njama ya kuwa mpatanishi, waendesha mashtaka walisema.

Benzema amekuwa akikanusha madai hayo na kusisitiza kuwa alikuwa akijaribu tu kumsaidia Valbuena kujiondoa kutoka kashfa ya video hiyo iliyomtia hatarini