Champions League 2021/22: Matokeo ya wiki hii, Hali ilivyo kwenye jedwali

Muhtasari

•Kwa sasa Manchester City inaendelea kuongoza kundi A kwa pointi 12, Liverpool inaongoza kundi B kwa pointi 15, Ajax iko kilelenikundi C na pointi 15, Real Madrid ndio bora kundi D na pointi 12, Bayern inaongoza kundi E na pointi 15, United kundi F na pointi 10, Lille kundi G na pointi 8 huku Chelsea ikiwa bora kundi H na pointi 12.

Raheem Sterling
Raheem Sterling
Image: CHAMPIONS LEAGUE

Michuano ya kombe la Champions League hatimaye ilirejea wiki hii baada ya mapumziko ya wiki mbili.

Siku ya Jumanne klabu 16 zilijitosa viwanjani mbalimbali bara Ulaya ili kuboresha nafasi zao za kufuzu katika raundi ya 16.

Bayern Munich walipata ushindi wa 2-1 ugenini dhidi ya Dynamo Kyiv  kupitia mabao ya Kingsley Coman na Robert Lewandowski.

Mashetani wekundu walishiriki mechi ya kwanza katika kombe hilo chini ya mkufunzi mpya wa muda mfupi Michael Carrick na kupata ushindi wa 2-0 ugenini dhidi ya Villareal. Christiano Ronaldo na Jadon Sancho ndio walikuwa walengaji shabaha usiku wa Jumanne.

Chelsea waliendeleza fomu yao nzuri huku wakiangamiza Juventus kwa mabao manne bila jawabu ugani Stamford Bridge. Trevoh Chalobah, Recce James, Calum Hudson-Odoi na Timo Werner walifanikisha ushindi huo.

Mechi kati ya Barcelona na Benfica iliishia sare tasa, mechi kati ya Young Boys na Atlanta ikaishia sare ya 3-3 huku Malmo FF na Zenit St Petersburg wakifungana 1-1.

Sevilla waliwachapa Wolfsburg 2-0 huku Lille wakichapa Salzburg 1-0 nyumbani.

Mechi nane zaidi zilichezwa usiku wa Jumatano.

Besiktas walipoteza nyumbani 1-2 dhid ya Ajax, Inter Milan wakapata ushindi wa 2-0  nyumbani dhidi ya Shakhtar Donetsk mwendo wa saa tatu kasorobo.

Liverpool waliwazima Porto 2-0 nyumbani kupitia mabao ya Thiago Alcantara na Mohammed Salah. City walipata ushindi wa 2-1 dhidi ya PSG kupitia mabao ya Raheem Sterling na Gabriel Jesus huku Kylian Mbappe akifungia PSG bao la pekee.

Atletico Madrid walipoteza nyumbani dhidi ya AC Milan huku Real Madrid wakiwika ugenini dhidi ya Sherrif Tiraspol 3-0.

RB Leipzig ilipata ushindi mkubwa wa 5-0 ugenini dhidi ya Club Brugge KV huku Sporting Lisbon wakiangamiza Borrusia Dortmund 3-1  nyumbani.

Kwa sasa Manchester City inaendelea kuongoza kundi A kwa pointi 12, Liverpool inaongoza kundi B kwa pointi 15, Ajax iko kilelenikundi C na pointi 15, Real Madrid ndio bora kundi D na pointi 12, Bayern inaongoza kundi E na pointi 15, United kundi F na pointi 10, Lille kundi G na pointi 8 huku Chelsea ikiwa bora kundi H na pointi 12.