Barca yaaga dimba la ligi ya mabingwa

Muhtasari

• Barca hawajakosa katika hatua ya 16 bora tangu 2003-04, wakati hawakufuzu kwa mashindano hayo kabisa.

• Mchezo huo, uliochezwa katika hali ya theluji na bila mashabiki kwa sababu ya kuongezeka kwa visa vya Covid-19 nchini Ujerumani.

• Droo ya Ligi ya Europa itafanyika Jumatatu saa sita adhuhuri GMT huko Nyon, Uswizi na Barca itacheza na mmoja wa washindi wa pili wa Kundi la Ligi ya Europa

Image: BBC

Mabingwa mara tano wa Uropa Barcelona walishindwa na Bayern Munich na kukosa kufuzu kwa hatua ya maondoano ya Ligi ya Mabingwa kwa mara ya kwanza katika kipindi cha miaka 17.

Barca hawajakosa katika hatua ya 16 bora tangu 2003-04, wakati hawakufuzu kwa mashindano hayo kabisa.

Kubanduliwa huko kunaendeleza masaibu ya miamba hao wa Uhispania baada ya changamoto za kifedha kuwalazimisha kumwachilia gwiji wa klabu hiyo Lionel Messi kuondoka kwa uhamisho wa bure na kujiunga na Paris St-Germain msimu wa joto.

Barca walihitaji kusawazisha matokeo ya Benfica ili kusonga mbele, lakini timu hiyo ya Ureno ilishinda 2-0 nyumbani dhidi ya Dynamo Kyiv, na kuwaacha vijana wa Xavi wakiwa nafasi ya tatu na kukabiliwa na mchujo wa hatua ya maondoano ya Ligi ya Europa.

Mchezo huo, uliochezwa katika hali ya theluji na bila mashabiki kwa sababu ya kuongezeka kwa visa vya Covid-19 nchini Ujerumani.

Bayern walifunga bao lao la kwanza wakati krosi ya Robert Lewandowski ilipomkuta Thomas Muller na mpira wake wa kichwa ukavuka mstari, kabla ya kuongeza bao kwa shuti kali la umbali wa yadi 30 kutoka kwa Leroy Sane.

Jamal Musiala aliongeza bao la tatu katika kipindi cha pili baada ya mkwaju wa Alphonso Davies.

Bayern wanasonga mbele kama washindi wa kundi wakiwa na rekodi ya 100%. Benfica ilimaliza kwa pointi nane, huku Barcelona, ​​ambao walifunga mara mbili pekee katika hatua nzima ya makundi, wakiwa na pointi saba.

Droo ya Ligi ya Europa itafanyika Jumatatu saa sita adhuhuri GMT huko Nyon, Uswizi na Barca itacheza na mmoja wa washindi wa pili wa Kundi la Ligi ya Europa, huku Rangers wakiwa mmoja wa wapinzani wao watarajiwa.