Wachezaji wanane wa Tottenham wapatikana na corona

Muhtasari

•Spurs wamepangiwa kucheza mechi dhidi ya Rennes katika michuano ya Ligi Europa siku ya Alhamisi na Uefa inasema "mechi hiyo itaendelea kama ilivyopangwa".

Meneja wa Tottenham Antonio Conte
Meneja wa Tottenham Antonio Conte
Image: GETTY IMAGES

Mkufunzi wa Tottenham Antonio Conte anasema wachezaji wanane na maafisa watano wa klabu hiyo wamepatikana na ugonjwa wa Covid-19.

Spurs wamepangiwa kucheza mechi dhidi ya Rennes katika michuano ya Ligi Europa siku ya Alhamisi na Uefa inasema "mechi hiyo itaendelea kama ilivyopangwa".

Baada ya hapo watachuana na Brighton Jumapili katika mechi ya Ligi Kuu ya England ambayo inaaminiwa kuwa inafanyiwa tathmini.

"Kila siku watu zaidi wanathibitishwa kuwa na virusi," alisema Conte.

"Hali sio nzuri kabisa."

Kufuatia mchezo dhidi ya Brighton, Tottenham watamenyana na Leicester City tarehe 16 Desemba na Liverpool tarehe 19 Disemba katika ligi ya daraja la kwanza kabla ya robo fainali ya Kombe la EFL dhidi ya West Ham mnamo Disemba 22.

"Kuzungumzia soka leo haiwezekani. Hali ya mwisho ilinifadhaisha sana," alisema Muitaliano huyo.

"Hali ni mbaya, kuna maambukizi makubwa.

“Tunajiandaa kwa ajili ya mchezo dhidi ya Rennes, lakini ni mgumu sana.