John Terry arejea Chelsea kama mshauri wa wachezaji wadogo

Muhtasari

•Chelsea imethibitisha kurejea kwa kiungo huyo wa zamani katika klabu hio, huku wakimpa mamlaka ya ushauri wa ukocha katika klabu hio.

John Terry
John Terry
Image: Hisani

John Terry, Beki wa zamani wa Uingereza , Jumatano aliwahakikishia mashabiki wa Chelsea   kurejea kwake kwenye timu hio.

Terry alionyesha furaha kubwa katika ukurasa wake wa Twitter akitangaza kurejea kurejea kwake katika uongozi wa wachezaji wadogo wa timu hio.

Chelsea imethibitisha kurejea kwa kiungo huyo wa zamani katika klabu hio, huku wakimpa mamlaka ya ushauri wa ukocha katika klabu hio.

Terry, ambaye ana umri wa miaka 41 alichezea Chelsea katika zaidi ya mechi 700 kama mchezaji na bado akiwa nahodha  na kusaidia timu hio kutoa mataji mengi

The Blues ilitangaza uteuzi wake kwa taarifa Jumatano, huku mchezaji huyo akitarajiwa kuanza kazi mara moja 

Beki huyo wa zamani wa Uingereza atachukua nafasi ya ushauri wa ukocha katika Akademi ya  Blues,  ambapo atakuwa akisaidia wachezaji wadogo pamoja na wakufunzi katika klabu hiyo ambapo alianzia tasnia yake ya kusakata kabumbu na kuibuka beki wa kusifika duniani

Jukumu la Terry katika klabu litahusisha kufundisha uwanjani, mijadala ya ukocha, ushauri wa wachezaji, pamoja na mazungumzo na wazazi. 

Uteuzi huu umegandia baada yake kuondoka Aston Villa  mapema mwaka.

 Terry alisaidia timu ya Chelsea kuibuka na kombe la primia Mara 5, tatu ikiwa chini ya Jose Mourinho, moja chini ya Carlo Ancelotti na moja chini ya Antonio Conte.