Mchezaji wa Chelsea, Romelu Lukaku Jumanne alijitokeza wazi na kuomba msamaha mashabiki wa Chelsea kwa Maneno aliyosema kuhusi ujio wake kwenye Klabu hio.
Lukaku ambaye alikosa Mechi ya Wikendi baina ya Chelsea na Liverpool, ambayo ilishia sare ya kufungana 2-2. Alisema anajuta kwa maneno aliyoyasema kwenye kituo cha Sky siku ya Jumatano
"Kwa mashabiki, samahani kwa usumbufu niliosababisha Nyinyi mnajua uhusiano nilionao na klabu hii tangu ujana wangu, kwa hivyo ninaelewa kabisa hayo." Lukaku alisema kupitia mtandao wa Timu hio.
Aliendelea kuomba Kocha,Thomas Tuchel msamaha na kuhakikisha ako tayari kujituma kusaidia timu hio kufikia marengo yao ya msimu huu.
"Kwa meneja, naomba radhi, na pia kwa wachezaji wenzangu na bodi nisameheni , kwa sababu nadhani haikuwa wakati sahihi. pia ninataka kwenda mbele kutoka kwa hili jambo na kuhakikisha kuwa tunaanza kushinda michezo yetu"