Everton yamtimua meneja wake Rafa Benitez

Muhtasari

•Ametimuliwa kufuatia msururu wa matokeo hafifu ambayo klabu hiyo imekuwa ikiandikisha hivi karibuni

Rafa Benitez
Rafa Benitez
Image: EVERTON

Klabu ya EPL ya Everton imesitisha mkataba wake na meneja wake Mhispania Rafael Benitez baada ya miezi saba tu.

Benitez ambaye alisajiliwa na Everton mwaka jana baada ya kuondoka kwa aliyekuwa meneja Carlo Ancelloti ametimuliwa kufuatia msururu wa matokeo hafifu ambayo klabu hiyo imekuwa ikiandikisha hivi karibuni.

Everton ilithibitisha kuondoka kwa Benitez siku ya Jumapili kupitia tovuti rasmi ya klabu huku ikitangaza kwamba mridhi wake atatafutwa hivi karibuni.

Hatua hii imejiri siku moja tu baada ya klabu hiyo kupoteza ugenini, 2-1 dhidi ya Norwich City  na kuongeza shinikizo kwa Benitez kutimuliwa.

Everton kwa sasa imekalia nafasi ya kumi na sita ikiwa na pointi 19 baada ya kuwa imeshiriki katika mechi 19 za EPL 2021/22.

Msimu uliopita klabu hiyo ilimaliza katika nafasi ya kumi ikijizolea pointi 59.