Algeria yabanduliwa nje ya AFCON kwa kichapo cha mabao 4-1

Muhtasari

• Algeria imeyaaga rasmi mashindano ya Kombe la Mataifa ya Afrika AFCON 2021 baada kupokezwa kichapo cha magoli 4-1 na timu ya Ivory Coast.

• Algeria ambao ni mabingwa watetezi wamebaduliwa kwenye hatua za makundi  kufuatia matokea mabaya waliyoandikisha  kwenye michuano hio

Nicolas Pepe akifunga bao la kwanza la Ivory coast
Nicolas Pepe akifunga bao la kwanza la Ivory coast
Image: twitter/Afcon

Timu ya Taifa ya Algeria imeyaaga rasmi mashindano ya Kombe la Mataifa ya Afrika AFCON baada kupokea kichapo cha magoli 4-1 kutoka kwa timu ya Ivory Coast.

Algeria ambao ni mabingwa watetezi walibaduliwa kwenye hatua za makundi  kufuatia matokea mabaya waliyoandikisha  kwenye michuano hio.

Msururu wa Algeria kutopoteza mechi 35 ulitiwa doa wakati walinyukwa na Equatorial Guinea katika matokeo yalioacha wengi vinywa wazi. 

Mechi baina yao na Ivory Coast ilikuwa ya kutamatisha michuano ya makundi huku wakiwa na matumaini ya kufuzu kwa awamu ya maondoano.

Nicolas Pepe mchezaji wa Arsenal aliipa uongozi Ivory Coast, kipindi cha kwanza huku Frankie Kessie, Ibraham Sangare, na Sebastien Haller pia wakifunga bao moja moja mtawalia na kusaidia Ivory Coast kumaliza kileleni mwa kundi hilo kwa pointi saba.

Wakifuatwa na Equatorial Guinea kwa pointi sita. Algeria  walipewa penalti wakapoteza kupitia mchezaji anayecheza kabumbu ya kulipwa nchini Uingereza, Riyad Mahrez.

 

Mhariri: Davis Ojiambo