Simba yakabwa koo na Kagera Sugar

Muhtasari

• Klabu ya Simba sports club Jumatano tarehe 26/01/2022 ilichabangwa bao moja komboa ufe dhidi ya Kagera Sugar, katika mtanange wa ligi kuu nchini Tanzania.

• Hadi dakika ya mapumziko, miamba hao wawili walikuwa bado hawajashuhudia bao katika lango la mwenzie.

• Sasa Simba wanasimama alama 10 nyuma ya wapinzani wao wa jadi Young Africans (Yanga) ambao wanaongoza jedwali kwa alama 35.

simba sports club, instagram
simba sports club, instagram
Image: kwa HISANI

Klabu ya Simba sports club Jumatano tarehe 26/01/2022 ilichabangwa bao moja komboa ufe dhidi ya Kagera Sugar, katika mtanange wa ligi kuu nchini Tanzania.

Hadi dakika ya mapumziko, miamba hao wawili walikuwa bado hawajashuhudia bao katika lango la mwenzie.

Mchezaji Kizza alipata nafasi na kuifungia Kagera Sugar bao moja na la kipekee kunako dakika ya 71. Baada ya ushindi huo, Kagera Sugar inashikilia nafasi ya 9 na alama 16 ,huku Simba ikitinga nafasi ya pili na alama 25.

Awali kabla ya mechi hiyo, mashabiki wa Simba walikuwa wameandaa maombi ya pamoja ili wapate ushindi katika mchuano huo.

Sasa Simba wanasimama alama 10 nyuma ya wapinzani wao wa jadi Young Africans (Yanga) ambao wanaongoza jedwali kwa alama 35.

Wengi wa mashabiki wanadadisi kuwa wachezaji wa Simba wamekosa confidence waliyokuwa nayo msimu wa jana, hii ikikisiwa kuwa baada ya aliyekuwa msemaji wao Hajji Manara kugura na kuingia Yanga.

Usimamizi wa Simba umesema kwamba wachezaji wao watajitahidi kurekebisha makosa waliyoyafanya na kusajili matokeo mazuri katika mechi zifuatazo.