Mshambulizi wa United Mason Greenwood ashtumiwa kwa unyanyasaji wa kinyumbani

Muhtasari

•Bi Robson alitumia ukurasa wake wa Instagram kutoa madai hayo dhidi ya Greenwood huku akiambatanisha na picha na video zilizoonyesha mwili wake ukiwa umechubuka.

Mshambulizi wa United Mason Greenwood ashtumiwa kwa kosa la unyanyasaji wa kinyumbani
Mshambulizi wa United Mason Greenwood ashtumiwa kwa kosa la unyanyasaji wa kinyumbani
Image: HISANI

Mshambulizi  matata wa Manchester United Mason Greenwood ameshutumiwa kwa kosa la  unyanyasaji wa kinyumbani na mpenzi wake Harriet Robson.

Bi Robson alitumia ukurasa wake wa Instagram kutoa madai hayo dhidi ya Greenwood huku akiambatanisha na picha na video zilizoonyesha mwili wake ukiwa umechubuka.

"Kwa kila mtu ambaye angetaka kujua ni nini Mason Greenwood hunanifanyia" Robson alinukuu video iliyoonyesha damu ikitirirka kutoka usoni mwake.

Wanamitandao haswa mashabiki wa soka na wanaopigana dhidi ya unyanyasaji wa kinyumbani wameendelea kutoa hisia tofauti huku uchunguzi na taarifa rasmi kutoka kwa mchezaji huyo na klabu ya United ukisubiriwa.

Kupitia kwa msemaji wao, Mashetani Wekundu wamesema uchunguzi unaendelea ili kubaini ukweli huku klabu hiyo ikisisitiza haikubaliani na unyanyasaji wa kinyumbani.

"Tunafahamu kuhusu picha na tuhuma zinazosambaa kwenye mitandao ya kijamii. Hatutatoa maoni yoyote zaidi hadi ukweli utakapothibitishwa. Manchester United haikubaliani na vurugu za aina yoyote.”" Taarifa ya United imesema.

Iwapo madai hayo yatabainika kuwa ya kweli, mshambuliaji huyo anahatarisha  kufungwa jela na kufukuzwa kutoka klabu ya United.