Dili zilizokamilika siku ya mwisho ya dirisha la uhamisho wa wachezaji la Januari

Muhtasari

•Uhamisho mkubwa zaidi ambao ulifanyika usiku wa mwisho wa mwezi Januari ni ule wa mshambulizi matata wa Gabon Pierre Emerick Aubameyang kuondoka Arsenal na kujiunga na Barcelona

Dili zilizokamilika siku ya mwisho ya dirisha la uhamisho la Januari
Dili zilizokamilika siku ya mwisho ya dirisha la uhamisho la Januari
Image: HISANI

Soko la uhamisho wa wachezaji barani Ulaya haswa Uingereza lilikuwa na shughuli nyingi mnamo siku ya mwisho ya dirisha la uhamisho la Januari.

Zaidi ya wachezaji kumi waliondoka ama kujiunga na klabu mbalimbali za ligi kuu Uingereza kabla ya siku ya Januari 31 kuisha.

Uhamisho mkubwa zaidi ambao ulifanyika usiku wa mwisho wa mwezi Januari ni ule wa mshambulizi matata wa Gabon Pierre Emerick Aubameyang kuondoka Arsenal na kujiunga na Barcelona ya Uhispania.

Aubameyang anaripotiwa kuondoka Arsenal kwa uhamisho huru baada ya klabu hiyo kujiondoa kwenye mazungumzo na wenzao wa Laliga na kumuachilia huru.

Hizi hapa dili zingine zilizokamilika mnamo siku ya mwisho ya dirisha la uhamisho la Januari:-

Donny Van De Beek (Manchester United-Everton)

Kiungo wa Manchester United Donny Van De Beek ambaye ni mzaliwa wa Uholanzi alijiunga na Everton kwa mkopo wa miezi kadhaa ambao utakamilika mwisho wa msimu wa 2021/22.

Delle Ali (Tottenham-Everton)

Mshambulizi Delle Ali hatimaye aliondoka Tottenham baada ya kuichezea kwa zaidi ya miaka saba na kujiunga na Everton.

Mzaliwa huyo wa Uingereza anaripotiwa kugharimu Toffees takriban pauni milioni 40.

Christian Eriksen (Brentford)

Baada ya kukaa kwa kipindi kirefu bila kushiriki katika mechi za kandanda, kiungo wa zamani wa Tottenham ana Intermilan Christian Eriksen alitia saini mkataba wa miezi sita na klabu ya Brentford.

Matt Target (Aston Villa- Newcastle)

Beki Matt Target alijiunga na Newcastle kutoka Aston Villa kwa mkopo hadi mwisho wa msimu wa 2021/22.

Dan Burn (Brighton-Newcastle)

Beki Daniel Burn kutoka Uingereza alitia saini mkataba wa miaka miwili unusu na Newcastle baada ya kusajiliwa kutoka Brighton kwa pauni milioni 12.5.

Aaron Ramsey (Juventus-Rangers)

Kiungo wa zamani wa Arsenal Aaron Ramsey alisajiliwa na Rangers kutoka Juventus kwa mkopo utakaokamilika mwisho wa msimu wa 2021/22.

Neco Williams (Liverpool-Fulham)

Klabu ya Fulham ilimsajili beki wa Liverpool na raia wa Uingereza Neco Williams kutoka Liverpool kwa mkopo hadi mwisho wa msimu wa 2021/22.

Dejan Kulusevski  (Juventus-Tottenham) 

Mshambulizi wa Juventus Dejan Kulusevski alijiunga na Tottenham kwa mkopo hadi mwisho wa msimu huu.