Kiungo Mukangula ndiye mchezaji bora wa mwezi Desemba wa AFC Leopards

Muhtasari

Kiungo wa kati wa timu ya AFC Leopards Eugine Mukangula ameibuka mchezaji bora wa mwezi Disemba wa timu hiyo inayoshiriki ligi kuu ya soka nchini Kenya.

Kiungo Eugine Mukangula akipokea zawadi ya mchezaji bora wa Disemba
Image: AFC Leopards (Facebook)

Kiungo wa kati wa timu ya AFC Leopards Eugine Mukangula ameibuka mchezaji bora wa mwezi Disemba wa timu hiyo inayoshiriki ligi kuu ya soka nchini Kenya.

Chingwe imetangaza haya Februari 1 na kusema kwamba katika kura zilizopigwa, Mukangula aliibuka mshindi huku akifuatiwa kwa ukaribu na wachezaji wenza Dan Musamali na Brian Wanyama.

Mukangula hadi sasa ndiye mfungaji bora wa timu ya AFC Leopards kwa mabao Matano, na amekuwa katika ubora wa kipekee uwanjani, huku akiisaidia Ingwe kupanda hadi nafasi ya kumi na mbili kwenye jedwali.

Kufuatilia ushindi huo, Mukangula anazawidiwa shilingi elfu 25 pamoja na kombe lililobinafsishwa kwa jina lake.

Kiungo huyo mahiri wa AFC Leopards pia anatarajiwa kuwania tuzo za mchezaji bora wa mwezi Januari baada ya kuwa na ustawi mkubwa kwenye mechi za Ingwe tangia mwaka wa 2022 kuanza.