Misri yazamisha Cameroon kuingia fainali

Muhtasari

•Misri walifuzu kuingia fainali ya Kombe la mabingwa  Afrika(AFCON) baada ya kuwapiga wenyeji Cameroon kwenye nusu fanaila iliyoishia kwa sare muda wa kawaida.

•Misri, ambao ni mabingwa mara saba wa Afrika  walianza  michuano  wakionekana kuzuazua kwenye hatua ya makundi ila wakaendelea kuimarika hadi kufikia fainali.

wachezaji wa Misri wakisherekea kutinga fainali
wachezaji wa Misri wakisherekea kutinga fainali
Image: twitter/Afcon2021

Misri walifuzu kwa fainali ya Kombe la mabingwa  barani Afrika (AFCON) baada ya kuwalaza wenyeji Cameroon katika nusu fainali iliyoishia kwa sare tasa muda wa kawaida.

Cameroon ambao wamekuwa na msururu wa matokeo mazuri waliondolewa kwenye michuano hiyo kupitia mikwaju ya penalti ambayo ilishia 3-1.

Misri, ambao ni mabingwa mara saba wa Afrika  walianza  michuano  wakionekana kusuasua kwenye hatua ya makundi ila wakaendelea kuimarika hadi kufika fainali.

Kocha wa Misri, Carlos Queiroz alionyeshwa kadi nyekudu na sasa atakosa mchuano wa fainali ambayo itachezwa Jumapili dhidi ya Senegal.

Huu ulikuwa  Mchezo wa  kwanza kuchezewa  uwanja wa Younde tangu mashabiki wanane kufariki kwenye lango la uwanja huo.

Fainali ya Jumapili itawakutanisha wachezaji wawili wa Livepool, Sadio Mane na Mohammed Sala.

Tunachosubiri ni kuona ni nani atanyakua kombe la mabingwa Afrika mwaka huu.