Nilijifunza! Pombe ilitishia kusambaratisha ndoa yangu - Wayne Rooney

Muhtasari

• Aliyekuwa mchezaji wa Manchester United na meneja wa sasa wa klabu ya Derby County, Wayne Rooney [36] amekiri kwamba utumizi wa vileo ulitishia kusambaratisha ndoa yake, kwa kile alikitaja kuwa alikuwa akifanya makosa mengi akiwa mlevi.

• Rooney amedokeza kwamba kwamba, kuna kipindi akiwa Old Trafford alibugia pombe kwa siku mbili mfululizo, jambo ambalo analijutia.

yeaahhh (1)
yeaahhh (1)

Aliyekuwa mchezaji wa Manchester United na meneja wa sasa wa klabu ya Derby County, Wayne Rooney [36] amekiri kwamba utumizi wa vileo ulitishia kusambaratisha ndoa yake, kwa kile alikitaja kuwa alikuwa akifanya makosa mengi akiwa mlevi.

Rooney amedokeza kwamba kwamba, kuna kipindi akiwa Old Trafford alibugia pombe kwa siku mbili mfululizo, jambo ambalo analijutia.

Hata hivyo Rooney amesisitiza kuwa yeye sio mlevi wa kutupwa bali alipitia kipindi cha mawazo mengi, hasira na matatizo ya afya ya akili ambavyo vilikuwa vikimuumiza sana.

Aidha ameongeza kuwa amekuwa na majadiliano ya kina na mkewe Coleen na alishamsamehe na pia alitafuta ushauri wa wataalamu ambao walimsaidia katika kutatua matatizo hayo.

Kwa sasa mkewe Coleen amemsihi mwanasoka huyo kuongozana na mtu mmoja (ambaye atachaguliwa na mkewe) kila anapokwenda kwenye sehemu za starehe ili kuhakikisha kuwa hajisahau na kufanya tabia zisizokuwa na maadili.