Beki Kurt Zouma ajipata mashakani baada ya kurekodiwa akimpiga paka wake teke ‘kama mpira’

Muhtasari

•Klabu yake ya West Ham imelaani kitendo chake na "itashughulikia suala hilo ndani".

Image: KURT ZOUMA

Mchezaji nyota wa Ligi Kuu ya Uingereza Kurt Zouma anaweza kufunguliwa mashtaka baada ya kurekodiwa kwenye picha ya video akimpiga paka wake kama mpira kwenye sakafu ya jikoni yake.

Nyota huyo wa West Ham, 27, pia anaonekana kumpiga kofi usoni paka huyo.

Klabu imelaani kitendo chake na "itashughulikia suala hilo ndani".

Beki huyo wa West Ham anaonekana akimshambulia mnyama huyo kwenye jumba lake la kifahari la pauni milioni 2 huku kaka yake akichukua video .

Zouma, mwenye umri wa miaka 27, anadondosha paka huyo na kisha kumpiga teke hewani kwenye sakafu ya jikoni.

Mfaransa huyo wa kimataifa kisha anamfukuza mnyama huyo kuzunguka chumba chake cha kulia chakula mbele ya mtoto huku mpigapicha akicheka.

Katika klipu ya mwisho, anaonekana akimpiga paka kwa nguvu usoni - na kutoka kwa mikono ya mtoto.

Jana usiku, Zouma aliomba radhi kwa shambulio hilo na kusisitiza kuwa lilikuwa tukio la pekee.

Alisema: “Nataka kuomba msamaha kwa vitendo vyangu. Hakuna visingizio kwa tabia yangu, ambayo ninajuta kwa dhati.