FIFA: Kenya yaporomoka hadi 103

Muhtasari

• Timu ya taifa Harambee Stars imeporomoka nafasi moja kutoka 102, hadi 103 katika msimamo wa FIFA uliotolewa mapema Februari 10.

• Barani Afrika, mabingwa wapya wa kombe la AFCON, Senegal wanazidi kudedea kileleni

• Belgium bado inazidi kushikilia nafasi ya kwanza kote duniani huku

Harambee Stars
Image: FACEBOOK

Timu ya taifa Harambee Stars imeporomoka nafasi moja kutoka 102, hadi 103 katika msimamo wa FIFA uliotolewa mapema Februari 10.

Harambee Stars imeporomoka baada ya kushindwa kufuzu michuano ya AFCON iliyokamilika wikendi iliyopita nchini Cameroon.

Barani Afrika, mabingwa wapya wa kombe la AFCON, Senegal wanazidi kudedea kileleni wakifuatiwa na Morocco, Nigeria, Misri na Tunisia wakifunga orodha ya timu za taifa tano bora barani Afrika kwa usanjari huo.

Katika msimamo huo wa FIFA, timu ya taifa ya Belgium bado inazidi kushikilia nafasi ya kwanza kote duniani huku ikifuatiwa na Brazil, Ufaransa, Argentina na Uingereza ikiwa imefunga tano bora kote duniani.

Katika ukanda wa Afrika mashariki, timu ya taifa ya Uganda inazidi kuongoza kwa kushikilia nafasi ya 84 kote duniani ikifuatiwa na timu ya Kenya (103), Tanzania (132), Rwanda (136), Burundi (141) huku Sudan Kusini ikiwa ya mwisho kwenye ukanda huu kwa kushikilia nafasi ya 168.

Kwa upande wa soka ya kina dada, Harambee Starlets inashikilia nafasi ya 145

Kuporomoka huku kwa timu ya taifa ya Kenya, Harambee Stars kulitarajiwa na wadadisi wengi wa soka nchini kwani kumekuwa na misukosuko katika uongozi wa soka nchini huku FKF ikimuachisha kazi aliyekuwa rais wa shirikisho hiloNick Mwendwa na Waziri wa Michezo Balozi Amina Mohammed akateua kamati ya mpito ili kuongoza shirikisho baada ya visa vya ufisadi kukumba uongozi wa awali wa shirikisho hilo.