Ni muujiza kurejea katika soka-Christian Eriksen

Muhtasari

•Mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 29 amefungwa kifaa cha maalum cha kuwezesha moyo wake kupiga cardioverter-defibrillator (ICD), baada ya kupatwa na mshtuko wa moyo.

Christian Eriksen asajiliwa na Brentford
Christian Eriksen asajiliwa na Brentford
Image: BRENTFORD

Christian Eriksen anasema ni muujiza kuweza kuanza tena soka akiwa na Brentford baada ya kuzimia alipokuwa akiichezea Denmark kwenye Euro 2020 msimu uliopita wa joto.

Mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 29 amefungwa kifaa cha maalum cha kuwezesha moyo wake kupiga cardioverter-defibrillator (ICD), baada ya kupatwa na mshtuko wa moyo.

Amejiunga na The Bees kwa mkataba wa miezi sita baada ya kuachiliwa na Inter Milan.

"Jambo la kwanza ni kuonesha shukrani," Eriksen aliiambia BBC Sport. "Kwa watu wanaonizunguka, wachezaji wenzangu, madaktari kwanza uwanjani, madaktari wa timu na wahudumu wa afya na kisha hospitalini, kufanya kila kitu na kuangalia kila kitu.

"Halafu ujumbe wote kutoka kwa watu kwa kuniunga mkono kwa yale ambayo familia yangu imepitia.

Imekuwa vizuri sana kuona ujumbe wa shukrani. "Nina bahati sana na nimewaambia ana kwa ana, nimefurahi sana wamefanya walichofanya vinginevyo nisingekuwa hapa."