Mzozo wa Ukraine: Poland yasusia mechi ya kufuzu kwa fainali ya Kombe la Dunia dhidi ya Urusi

Muhtasari

•Poland haitacheza mechi ya mchujo ya Kombe la Dunia la 2022 dhidi ya Urusi mjini Moscow mnamo Machi 24 kutokana na uvamizi wa Urusi dhidi ya Ukraine

Image: BBC

Poland haitacheza mechi ya mchujo ya Kombe la Dunia la 2022 dhidi ya Urusi mjini Moscow mnamo Machi 24 kutokana na uvamizi wa Urusi dhidi ya Ukraine, rais wa shirikisho la soka la Poland amesema.

"Hakuna maneno zaidi, ni wakati wa kuchukua hatua," Cezary Kulesz alisema. Alisema Poland ilikuwa inazungumza na mashirikisho ya soka ya Czech na Uswidi ili kuwasilisha msimamo mmoja kwa shirikisho la soka duniani FIFA.

Urusi inatazamiwa kuwa mwenyeji wa Poland mjini Moscow tarehe 24 Machi, huku Ukraine ikisafiri hadi Scotland siku hiyo hiyo.

Wakati huo huo kiungo wa kimataifa wa Poland Robert Lewandowski ameunga mkono hatua ya nchi yake kususia mechi ya kufuzu kwa fainali ya Kombe la Dunia dhidi ya Urusi baada ya uvamizi wa Ukraine, akisema "hatuwezi kujifanya kuwa hakuna kinachoendelea".

Mshambulizi huyo wa Bayern Munich Lewandowski, 33, ambaye ni mfungaji bora wa mabao nchini mwake, aliongeza: "Siwezi kucheza mechi na timu ya taifa ya Urusi wakati nchi hiyo ikiendelea na uvamizi wake dhidi ya Ukraine.