Roman Abramovich avuliwa ukurugenzi Chelsea

Muhtasari

•Kamati ya Ligi kuu ya Uingereza imechukua hatua hiyo kumuondoa kutoka klabu hicho kufuatia uamuzi serikali ya Uingereza kumuwekea tajiri huyo vikwazo .

•Serikali inaamini kuwa bilionea huyo amekuwa na "uhusiano wa karibu kwa miongo kadhaa" na rais wa Urusi Vladimir Putin.

Mmiliki wa Chelsea Roman Abramovich
Mmiliki wa Chelsea Roman Abramovich
Image: BBC

Ligi Kuu ya Uingereza ( EPL) imemuondoa mmiliki wa Chelsea Roman Abramovich kuwa mkurungezi wa Klabu hiyo.

Kamati ya Ligi kuu ya Uingereza imechukua hatua hiyo kumuondoa kutoka klabu hicho kufuatia uamuzi serikali ya Uingereza kumuwekea tajiri huyo vikwazo kama njia ya kuijibu Urusi kwa kuivamia Ukraine.

Kwa sasa Chelsea imepatiwa kibali maalum cha kuhudumu na kuendelea na shughuli za mpira hata baada ya mali ya Abramovich kupigwa tanji na serikali ya Uingereza.

Ligi Kuu ya uingereza inasema ingawa Abramovich amepigwa marufuku lakini hatua hiyo "haitaathiri Chelsea kufanya mazoezi na kusakata mpira"

Bilionea huyo amekuwa akiiongoza klabu hiyo tangu 2003 lakini majaribio yake ya kutaka kuiuza klabu hiyo yalisitishwa na serikali ya Uingereza, ambayo imezuia mali yake

Abramovich aliwekewa vikwazo na serikali ya Uingereza siku ya alhamisi iliyopita kama sehemu ya majibu yake kwa uvamizi wa Urusi dhidi ya Ukraine.

Serikali inaamini kuwa bilionea huyo amekuwa na "uhusiano wa karibu kwa miongo kadhaa" na rais wa Urusi Vladimir Putin, viungo ambavyo Abramovich amekuwa akikanusha.

Mbali na yaliompata tajiri Abramovich klabu chake cha Chelsea nacho kitakuwa chini ya marufuku ya uhamisho ikimaanisha kuwa haiwezi kununua wala kuuza wachezaji.

Chelsea vilevile haitaruhusiwa kujadili mikataba mipya kwa wachezaji wake, meneja na wafanyakazi wake wote.