Wezi wavunja na kupora nyumbani kwa mchezaji Paul Pogba

Muhtasari

• Mchezaji wa Manchester United, Paul Pogba amesema kwamba wezi walivamia na kupora nyumbani kwake alipokuwa akishiriki mechi dhidi ya Atletico Madrid.

• "Jana usiku familia yangu ilipatwa na jinamizi kubwa zaidi baada ya wezi kuvamia na kupora nyumbani kwetu, huku watoto wakiwa wamelala," Pogba aliandika.

Paul Pogba
Paul Pogba
Image: GETTY IMAGES

Mchezaji wa Manchester United, Paul Pogba amesema kwamba wezi walivamia na kupora nyumbani kwake alipokuwa akishiriki mechi dhidi ya Atletico Madrid.

Kupitia ujumbe aliochapisha katika ukurasa wa Twitter, Pogba alisema kwamba kitendo hicho kilifanyika huku wanawe wakiwa wamelala chumbani mwao.

"Jana usiku familia yangu ilipatwa na jinamizi kubwa zaidi baada ya wezi kuvamia na kupora nyumbani kwetu, huku watoto wakiwa wamelala," Pogba aliandika.

Staa huyo wa mpira wa miguu alikiri kwamba wezi hao walikuwa nyumbani kwa dakika tano tu ila yeye, mkewe na wanawe wameachwa na wasiwasi ya usalama wao tangu hapo.

Kulingana naye, tukio hilo lilifanyika dakika za mwisho za mechi yao ya raundi ya 16 bora dhidi ya Atletico Madrid ambapo walijua kwamba hawangekuwepo nyumbani.

"Mimi na mke wangu tulikimbia nyumbani bila kujua iwapo wanetu wako salama na bila kujeruhiwa," Pogba aliandika.

Pogba alisema kwamba kama baba anahisi vibaya kwamba hakuwepo kuwakinga watoto wake dhidi ya wezi hao na kusema kwamb hangetaka mtu yeyote kupitia hali hiyo.

Paul Pogba  aliahidi kutoa zawadi  kwa shabiki ambaye atatoa ripoti yoyote kuhusu wezi hao itakayosidia pia katika uchunguzi