Louis Van Gaal apatikana na prostate cancer

Muhtasari

• Louis Van Gaal amepatikana na ugonjwa wa prostate cancer.

• Alisema kwamba ufanisi wake kimaisha umechangiwa pakubwa na hali hizo, ndo maana nikaona itakuwa bora zaidi kuandaa makala maalum.

kocha wa Uholanzi, Louis Van Gaal
kocha wa Uholanzi, Louis Van Gaal
Image: Manchester United [Facebook]

Meneja wa timu ya taifa ya Uholanzi Louis Van Gaal amefichua kwamba anaugua ugonjwa wa prostate cancer.

Van Gaal, 70, alikiri hayo katika mahojiano kwenye kipindi cha #Humberto Jumapili alipokuwa akipigia debe makala aliyoyaandaa kuhusu maisha yake.

Mkufunzi huyo alisema kwamba wachezaji wake hawafahamu kuhusu hali hiyo.

"Nimepitia mengi kutokana na ugonjwa, ikiwemo maisha yangu mwenyewe. Kwa hiyo nishakubali hali hiyo kuwa sehemu ya maisha yangu," Van Gaal alisema.

Alisema kwamba ufanisi wake kimaisha umechangiwa pakubwa na hali hizo, ndo maana nikaona itakuwa bora zaidi kuandaa makala maalum.

Ikumbukwe kwamba Van Gaal alichukuwa mikoba ya kuinoa Uholanzi kwa awamu ya tatu mnamo mwezi Agosti mwaka wa 2021, akiwa amewaongoza miamba hao kumaliza  nafasi ya tatu katika kombe la dunia mwaka wa 2014.

Alikuwa amechukua nafasi yake Frank de Boer baada ya matokeo mabaya kwenye kipute cha Euro 2020 ambapo Uholanzi walibanduliwa katika awamu ya kumi na sita bora.

Mwalimu huyo ambaye aliwahi kuinoa Manchester United, anatarajiwa kuiongoza Uholanzi katika kombe la dunia mwaka huu kule Qatar.