Ramadhan 2022: Jinsi soka ya Ligi Kuu inavyobadilika ili kuwasaidia wachezaji Waislamu

Kuna mechi tisa za jioni ambazo huenda wachezaji wakahitaji kufuturu wakati wa mchezo.

Muhtasari

•Mfungo wa Ramadhan nchini Uingereza utaanza katu ta 04:00 na 05:00 BST na kumalizika kati ya 19:30 na 20:30 kadri siku zinavyosonga.

Baadhi ya wachezaji wa Kiislamu watalazimika kufungua muadhini wakati wa mechi za jioni za Ligi Kuu wakati huu wa Ramadhan
Baadhi ya wachezaji wa Kiislamu watalazimika kufungua muadhini wakati wa mechi za jioni za Ligi Kuu wakati huu wa Ramadhan
Image: BBC

Unaweza kuona mabadiliko kidogo katika baadhi ya mechi za Ligi Kuu katika wiki chache zijazo.

Hii ni kwa sababu Waislamu kote duniani wanaadhimisha mfungo wa Ramadhan kwa mwezi mmoja, kilele chake ikiwa ni sherehe za Eid mnamo Mei 2.

Mfungo wa Ramadhan nchini Uingereza utaanza katu ta 04:00 na 05:00 BST na kumalizika kati ya 19:30 na 20:30 kadri siku zinavyosonga.

Hii inamaanisha mechi 52 ya Ligi Kuu iliyopangwa kufanyika mwezi wa Ramadhani, kuna mechi tisa za jioni ambazo huenda wachezaji wakahitaji kufuturu wakati wa mchezo.

Msimu uliopita katika mechi kati ya Leicester City na Crystal Palace kwenye Uwanja wa King Power Stadium, ilisitishwa kwa muda ili kumruhusu beki wa Foxes Wesley Fofana na kiungo wa Eagles, Cheikhou Kouyate kufanya hivyo.

Wesley Fofana wa Leicester pia lifungua mfungo wake wakati wa mechi dhidi ya Southampton msimu uliopita kwa kula ndizi wakati wa mapumziko.
Wesley Fofana wa Leicester pia lifungua mfungo wake wakati wa mechi dhidi ya Southampton msimu uliopita kwa kula ndizi wakati wa mapumziko.
Image: GETTY IMAGES

Je nini kitafanyika msimu huu?

Ibada na usomaji wa Kurani huongezeka wakati wa Ramadhani, pamoja na kutoa sadaka kwa hisani ili kuimarisha imani ya Muumini wa Kiislamu.

Lakini lengo kuu ni kufunga - kuacha kula au kunywa wakati wa mchana - ambayo inaleta changamoto kwa wanasoka wa Kiislamu ambao wana mwelekeo wa kubadilisha mafunzo yao ili kukabiliana na ukali wa mwezi.

Msimu uliopita, kulikuwa na makubaliano yasiyo rasmi kati ya manahodha kuruhusu mapumziko mafupi kwenye goli au kurusha ndani ili wachezaji wowote Waislamu wanaohitaji waweze kufuturu.

Msimu huu, ingawa kumekuwa hakuna mwongozo rasmi kwa timu za daraja la juu kwani hauathiri kila mchezo, manahodha wanaweza tena kuomba mapumziko ya vinywaji wakati mwafaka katika mchezo wakati wa mkutano wao wa kabla ya mechi na waamuzi.

Jua likishatua, itawaruhusu wachezaji wanaofunga kuja kando ya uwanja na kupata vinywaji kwa au virutubishi vyovyote kabla ya kuanza tena mchezo.

Ili kupata uelewa mzuri zaidi kuhusu misingi ya Ramadhani, wanachama wa Professional Game Match Officials Limited (PGMOL) wamepewa nafasi ya kufanya warsha itakayoongozwa na Nujum Sports siku ya Ijumaa.

Ni mechi gani zinaweza kuathiriwa?

Mechi zifuatazo za jioni zinaweza kuwa na wachezaji wa Kiislamu watakaochezea timu zao wakiwa wamefunga:

Jumatatu, Aprili 4: Crystal Palace v Arsenal (20:00)

Jumatano, April 6: Burnley v Everton (19:30)

Ijumaa, Aprili 8l: Newcastle v Wolves (20:00)

Jumanne, Aprili 19: Liverpool v Manchester United (20:00)

Jumatano, Aprili 20: Chelsea v Arsenal, Everton v Leicester, Newcastle v Crystal Palace (zote zitachezwa19:45), Manchester City v Brighton (20:00)

Alhamisi, April 21: Burnley v Southampton (19:45)

'Sio kila mtu anapaswa kufunga...'

Makasisi wa Kiislamu katika Michezo wameandika kijitabu cha habari cha Ramadhani ambacho kimeidhinishwa na kusambazwa na Ligi Kuu
Makasisi wa Kiislamu katika Michezo wameandika kijitabu cha habari cha Ramadhani ambacho kimeidhinishwa na kusambazwa na Ligi Kuu
Image: MCS

Makasisi wa Kiislamu katika Michezo wameandika kijitabu cha habari cha Ramadhani ambacho kimeidhinishwa na kusambazwa na Ligi Kuu.

Wazee, wagonjwa na wanawake wajawazito, wanaonyonyesha au wanaopata hedhi hawalazimiki kufunga.

Yeyote anayesafiri umbali wa zaidi ya maili 48 (kilomita 80) pia ameruhusiwa kula, lakini lazima alipe saumu baadaye, kwa hivyo hii inajumuisha wachezaji wanaoenda kwenye michezo ya ugenini.

Muslim Chaplains in Sport (MCS) ilianzishwa mwaka wa 2014 na ndilo shirika pekee la aina yake kuidhinishwa na kufadhiliwa na Premier League na EFL, likifanya kazi katika vilabu vyote 92 vya taaluma ya kandanda kutoa mihadhara na semina za elimu.

Vilabu vya Ligi Kuu ya Uingereza mara kwa mara hutafuta mwongozo wa Kiislamu kutoka kwa MCS kwa niaba ya wachezaji wao Waislamu, ikiwa ni pamoja na masuala kama vile kuahirisha mifungo ili uchezaji wao wa mazoezi na wakati wa mechi usiathiriwe.

"Ingawa hakuna uamuzi wa Kiislamu kwa wanariadha, tunatoa ushauri kuhusu jinsi wanavyoweza kudumisha imani zao na kujadili kama wanafuzu kusamehewa, kama vile wanapokuwa safarini au wagonjwa," mkurugenzi mkuu wa MCS Ismail Bhamji aliambia BBC Sport.

"Wacheza kandanda wa Kiislamu wanatoka katika asili tofauti na inabidi tutafute suluhu ambazo zitafanya kazi kwa wote kutekeleza imani yao.

"Klabu moja ya Ligi Kuu iliniomba nizungumze na mchezaji Mwislamu ili kuahirisha mfungo wake wa Ramadhani. Kiislam hana sifa kwa sababu masharti fulani yaliyotajwa lazima yatimizwe na lazima niwe muwazi na mkweli kwao juu ya ukweli mbaya."

MCS inafanya kazi kwa karibu na klabu mbili kuu nchini, Manchester City na Liverpool, na Bhamji alitoa hotuba ya Ramadhani katika Kampasi ya Etihad siku ya Jumatano, huku pia akisifu mbinu zao za utofauti na kupanua ujuzi wao kuhusu masuala haya.

"City na Liverpool zinafanya vizuri zaidi na ninaona misingi iliyowekwa kwenye klabu hiz mbili," alisema. "Kuanzia chuo cha mafunzo na kuendelea, wana watu sahihi na wenye fikra sahihi na maono ya kusaidia klabu hadi kwenye kikosi cha kwanza.

"[Makocha] Pep Guardiola na Jurgen Klopp wanasifika kwa sababu wana maendeleo na wanafikiria mbele kwa hivyo nimeona maboresho yakifanywa katika kllabu kwa misimu kadhaa."