logo

NOW ON AIR

Listen in Live

Chelsea, Bayern Munich waiaga Champions League

Safari ya Bayern Munich ilifika ukingoni  baada ya kushindwa kupata ushindi nyumbani dhidi ya Villareal.

image
na Radio Jambo

Habari13 April 2022 - 02:31

Muhtasari


•Safari ya Bayern Munich ilifika ukingoni  baada ya kushindwa kupata ushindi nyumbani dhidi ya Villareal.

•Real Madrid iliponea chupuchupu kubanduliwa nje ya kombe hilo baada ya mshambulizi Rodrygo kufunga bao muhimu katika dakika ya 80.

Mabingwa mara sita wa Champions League Bayern Munich na mabingwa mara mbili Chelsea walipungia kombe hilo mkono wa kwaheri usiku wa Jumanne katika mkondo wa  robo fainali.

Safari ya Bayern Munich ilifika ukingoni  baada ya kushindwa kupata ushindi nyumbani dhidi ya Villareal.

Mechi hiyo ambayo ilichezwa mwendo wa saa nne usiku iliisha kwa sare ya 1-1 hivyo kufanya jumla ya mabao kuwa Bayern 1, Villareal 2. Vijana wa Unai Emery walipata ushindi wa 1-0 katika mechi ya mkondo wa kwanza.

Real Madrid iliponea chupuchupu kubanduliwa nje ya kombe hilo baada ya mshambulizi Rodrygo kufunga bao muhimu katika dakika ya 80.

Bao la Rodrygo lilifanya mchuano huo uende hadi dakika za maongezi ambapo Benzema alifungia Madrid bao la pili na kuipa klabu hiyo ya Uhispani ushindi wa 5-4 kwa jumla.

Villareal na Real Madrid wanasubiri kujua washindani wao katika nusu fainali ambao watapatikana kutoka kwa mechi mbili zitakazochezwa usiku wa Jumatano.

Atletico Madrid watakaribisha Manchester City ugani Wanda Metrapolitano mwendo wa saa nne huku Benfica wakiwa wenyeji wa Liverpool ugani Anfield.


RADIO JAMBO FREQUENCIES

Kisumu 100.1 | Mombasa 92.3 | Nakuru 96.9 | Eldoret 99.5 | Nyeri 99.3 | Nyahururu 97.3 | Webuye 95.3 | Meru 92.7 | Kitui 104.9 | Kibwezi 104.7 | Voi 105.7 | Malindi 98.1 | Lamu 104.7 | Narok 97.3 | Kapenguria 99.7 | Kisii 89.3 | Garissa 104.3 | Maralal 97.3 | Lodwar 92.7


logo© Radio Jambo 2024. All rights reserved