Real Madrid yaongoza kwa kuwa na 'chapa' yenye thamani kubwa zaidi duniani

Muhtasari
  • Klabu ya Real Madrid ya Hispania imeendelea kushika usukani wa kuwa chapa yenye thamani kubwa zaidi duniani kwa miaka minne mfululizo

Klabu ya Real Madrid ya Hispania imeendelea kushika usukani wa kuwa chapa yenye thamani kubwa zaidi duniani kwa miaka minne mfululizo.

Kwa mujibu wa Brand Finance Football 50 2022, Real Madrid ndiyo chapa yenye thamani kubwa zaidi ya soka duniani kwa mwaka wa nne mfululizo.

Ripoti kutoka The Football 50 2022 inaitaja thamani ya chapa ya klabu hiyo kwa sasa kufikia €1.5 bilioni na kuzipiku Klabu za Manchester City (€1.3bn) na Barcelona (€1.3bn).

Katika ripoti yake, Brand Finance inabainisha kuwa, "Ongezeko la thamani ya chapa ya Real Madrid mwaka huu lilitokana na mchanganyiko wa nguvu ya chapa yenyewe iliyoboreshwa na mwelekeo mzuri wa mapato. Chapa hii ina fursa nzuri za kukua pamoja na fursa za ufadhili."

'Klabu inajivunia chapa yenye nguvu zaidi ya kandanda duniani', ilisema taarifa ya klabu hiyo kuhusu ripoti hiyo.

Brand Finance pia huamua nguvu ya chapa kupitia vipimo vinavyotathmini uwekezaji wa masoko, usawa wa wadau na ufanisi wa biashara.

Katika orodha hii, Real Madrid ilipata alama ya Brand Strength Index ya 94.0 kati ya 100 na alama ya chapa ya AAA+, ambayo inaweka klabu hiyo kuwa mbele ya Liverpool yenye alama (92.9) na Barcelona (92.1).

Orodha ya Vilabu 10 bora vyenye chapa yenye thamani zaidi duniani

1. Real Madrid €1.5bil

2. Manchester City €1.3bil

3. Barcelona€1.3bil

4. Liverpool€1.3bil

5. Manchester United€1.3bil

6. Bayern Munich€1.1bil

7. PSG €1.0bil

8. Tottenham€0.9bil

9. Chelsea€0.9bil

10. Arsenal€0.8bil

Brandi 10 bora za klabu zenye nguvu zaidi sokoni kwa mwaka 2022

Alama

1Real Madrid94.0

2Liverpool92.9

3Barcelona92.1

4Manchester United 92.0

5Bayern Munich88.6

6Manchester City87.7

7Juventus 86.1

8Arsenal 85.9

9Chelsea 84.7

10Tottenham83.1