Uhamisho wa EPL: Wafahamu wachezaji wanaosakwa zaidi

Muhtasari

• Ligi ya England inang'oa nanga tena tarehe 6 Agosti - chini ya wiki 10 zijazo-na kuna dalili kuwa itakuwa ni msimu wenye shughuli nyingi za soka.

Image: BBC

Msimu wa Primia Ligi ndio kwanza umekamilika , lakini tayari tumekwishashuhudia hatua za kuhama kwa kwa wachezaji katika soko la uhamisho huku klabu zikiangalia jinsi ya kuiba wachezaji watakaofaa klabu zao kutoka kwa mahasimu wao kabla ya msimu mpya.

Huku Kombe la Dunia la Msimu wa baridi likikaribia, Ligi ya England inang'oa nanga tena tarehe 6 Agosti - chini ya wiki 10 zijazo-na kuna dalili kuwa itakuwa ni msimu wenye shughuli nyingi za soka.

Kuhamia kwa Erling Haaland katika Manchester City, kumegonga vichwa vya habari mapema, huku kuhamia kwa Ivan Perisic katika Tottenham kutawafanya mashabiki wao kufurahi.

Shughuli ya uhamisho wa mapema unajumuisha ule wa Brenden Aaronson kutoka Leeds United anayehama kwa £25m, akielekea Red Bull Salzburg, uwezo wa Liverpool kumchukua Fabia Carvalho kutoka Fulham, na Aston Villa kuwachukua Diego Carlos na Boubacar Kamara.

Lakini huku makala ya tetesi ikiendelea kuvutia zaidi na tetesi kuhusu kuhamia England kutoka katika mabara mengine, BBC michezo inaangazia baadhi ya sura mpya tunazoweza kuzishuhudia katika msimu ujao.

Tufahamishe ni nani ungetaka klabu yako imsaini msimu huu.

Julian Alvarez

Julian Alvarezanatarajiwa kupigania kwa mara ya kwanza kupata nafasi katika ya kwanza ya Man City msimu huu
Julian Alvarezanatarajiwa kupigania kwa mara ya kwanza kupata nafasi katika ya kwanza ya Man City msimu huu
Image: BBC

Mshambuliaji wa Argentina anajiunga na Manchester City kutoka River Plate mwezi Januari. Bado hajaonekana mbele ya mashabiki wa soka Waingereza hatahivyo, baada ya kurudishwa kuchukuliwa kwa mkopo moja kwa moja na machampioni wa Argenina.

Akifahamika kwa jina bandia la 'Aguero mpya ' kwa baadhi, kuwasili kwa Alvarez katika kikosi cha City msimu huu kutafunikwa na uwepo wa Haaland lakini kuna fununu nyingi kwamba mchezaji huyu mwenye umri wa miaka 22 kuleta mafanikio makubwa katika Manchester.

Mkataba wa malipo ya £14.4m , wa mchezaji huyu ambaye zaidi ni mshambuliaji, lakini anayeweza kutamba maeneo tofauti ya uwanja, hivi karibuni alifunga mabao sita katika mechi ya Copa Libertadores na yalikuwa chini ya makubaliano ya mkataba wake.

Darwin Nunez

Darwin Nunez aliifunga Benfica mabao sita ya Championi Ligi msimu uliopita
Darwin Nunez aliifunga Benfica mabao sita ya Championi Ligi msimu uliopita
Image: BBC

Ni jina lililozoeleka sana katika makala ya tetesi za soka Ulaya na mshambuliaji ambaye bila shaka huvutia hisia za kupendwa kutoka katika klabu kadhaa za Primia Ligi

Mshambuliaji huyu wa Benfica aliifungia mabao klabu yake 34 katika mabao 43 ya mechi za msimu uliopita, yakiwemo sita katika Championi Ligi, na ameripotiwa kwa kiasi kikubwa kwamba atahama msimu huu licha ya kwamba mkataba miaka mitatu imesalia kwenye mktaba wake wa sasa na Benfica

Manchester United, Liverpool, Arsenal na Newcastle United zote zimehusishwa na taarifa za ku,mnunua kijana huyu mwenye umri wa miaka 22, lakini hatauzwakwa gharama ya chini, huku Benfica wakiripotiwa kumtaka kwa pauni milioni 100.

Christopher Nkunku

Christopher Nkunku alitajwa kama mchezaji wa msimu wa Ligi ya Bundesliga 2021-22
Christopher Nkunku alitajwa kama mchezaji wa msimu wa Ligi ya Bundesliga 2021-22
Image: BBC

Mshambuliaji mwingine wa kufurahisha ambaye anaweza kuwa anaelekea katika Primia Ligi ni Christopher Nkunku.

Chelsea na Manchester United zimekuwa zikihusishwa sana na mchezaji huyu wa Bundesliga wa msimu baada ya kufunga mabao 20 na kusaidia kufungwa kwa magoli 13 katika klabu yake ya Ujerumani ya Leipzig.

Mfaransa huyu mwenye umri wa miaka 24 anaripotiwa kulengwa na klabu yake ya zamani , Paris St-Germain, baada ya kuondoka katika klabu hiyo mwaka 2019.

Hugo Ekitike

Hugo Ekitike alikaribia kuhamia Newcastle katika mwezi wa Januari
Hugo Ekitike alikaribia kuhamia Newcastle katika mwezi wa Januari
Image: BBC

Newcastle ilionyesha nia katika mshambuliaji wa Reims mwezi Januari na pia klabu chache za Primia Ligi zinaweza kuwa kusaka saini ya mchezaji huyu mwenye umri wa miaka 19.

Liverpool na Aston Villa ni miongoni mwa klabu kubwa za England zinazohusishwa na mshambuliaji wa kikosi cha ufaransa cha vijana wenye chini ya umri wa miaka 20, ambaye''huenda akaondoka'' msimu huu, kulingana na rais wa klabu ya Reims ,Jean-Pierre Caillot.

Akiwa na magoli 11 na kusaidia kufunga mabao katika ligi 26 na kucheza michuano ya kombe katika upande wa Ligi ya 1 ya Ufaransa, Ekitike pia ni mchezaji anayetamaniwa kote Ulaya na anatarajiwa kugarimu pauni milioni 40.

Ousmane Dembele

Ousmane Dembelealikuwa ni mchezaji wa barcelona aliyeweka rekodi ya kusaini mkataba wa garama kubwa alipowasili kutoka Dortmund uliofikia pauni milioni 136 mwaka 2017
Ousmane Dembelealikuwa ni mchezaji wa barcelona aliyeweka rekodi ya kusaini mkataba wa garama kubwa alipowasili kutoka Dortmund uliofikia pauni milioni 136 mwaka 2017
Image: BBC

Dembele - ni mchezaji mwingine ambaye amekuwa akihusishwa katika siku za hivi karibuni na taarifa za kuhamia Liverpool, kuchukua nafasi ya Divock Origi anayeondoka kwenye klabu hiyo na uwezekano wa kuondoka kwa Sadio Mane.

Lakini Liverpool haitakuwa klabu pekee yenye nia na winga huyo wa barcelona mwenye umri wa miaka 25, ambaye ameripotiwa kuwa yuko tayari kuondoka Nou Camp.

huku mkataba wake wa sasa na Barca ukitarajiwa kumalizika msimu huu na kusaini makubaliano mapya kufikiwa, mchezaji huyi wa kimataifa wa Ufaransa -hivi karibuni akitarajiwa kuwa wakala huru -amekuwa akihusishwa na klabu za Chelsea , Manchester United na Paris St-Germain.

Dembele alihamia Barcelona kwa mkataba wa pauni milioni 136 kutoka Dortmund katika mwaka 2017, na amesaidia kufungwa kwa mabao 13 katika laliga na kucheza michezo 21 tangu Xavi ateuliwe kuwa meneja wa klabu hiyo mwezi Novemba.

Moussa Diaby

Moussa Diaby amecheza mchezo wa kufurahisha katika Bayer Leverkusen
Moussa Diaby amecheza mchezo wa kufurahisha katika Bayer Leverkusen
Image: BBC

Arsenal na Newcastle zimekuwa zikihusishwa sana na winga huyu wa Bayer Leverkusen, Diaby katika wiki za hivi karibuni kufuatia mchezo wake uliofurahisha katika msimu wa Bundasliga.

Mshambuliaji huyu- Mfaransa mwenye umri wa miaka 22-amekwishafunga mabao 17 msimu huu na alichangia kufungwa kwa magoli 31 katika mechi 43, huku ikijulikana kuwa Leverkusen wameazimia kutomuachilia.

Inaripotiwa kuwa pauni milioni 60 za ziada zinahitajika kumuondoa katika klabu hiyo ya Ujerumani.