Sadio Mane ajiunga rasmi na Bayern Munich hadi 2025

Muhtasari

• Nyota huyo wa Senegal ametia saini mkataba wa miaka mitatu na ujio wake unaonekana kama mapinduzi kwa vijana wa Julian Nagelsmann na Bundesliga.

• Usajili wake utapunguza maumivu kwa Bayern ikiwa mshambuliaji mtoro Robert Lewandowski ataondoka.

Bayern Munich wamemsajili Sadio Mane kutoka Liverpool, vilabu vyote viwili vimethibitishw a Jumatano, huku mshambuliaji huyo wa Senegal akisaini mkataba wa miaka mitatu na mabingwa hao wa Bundesliga.

Mane anaondoka baada ya misimu sita na klabu ya Liverpool ya Uingereza na kusakata jumla ya mechi 269 na kufikisha mabao 120.

Ada ya uhamisho inaripotiwa kuwa karibu dola milioni 43 kwa Mane, ambaye alishinda Ligi ya Mabingwa, Ligi ya Premia, Kombe la FA na Kombe la Dunia la Klabu kwa miaka sita huko Merseyside.

Nyota huyo wa Senegal ametia saini mkataba wa miaka mitatu na ujio wake unaonekana kama mapinduzi kwa vijana wa Julian Nagelsmann na Bundesliga.

"Nilichagua Bayern Munich kwa sababu ingawa nilikuwa na ofa zingine, ni wakati mwafaka wa kusonga mbele na kuja hapa," aliambia mkutano wa waandishi wa habari.

"Nilikutana na kocha (Nagelsmann) na kwangu, ilikuwa muhimu sana kujua mradi huo. Niliona nitachezea timu hiyo moja kwa moja na sikufikiria mara mbili."

Usajili wake utapunguza maumivu kwa Bayern ikiwa mshambuliaji mtoro Robert Lewandowski ataondoka katika klabu hiyo, huku winga wa Ujerumani Serge Gnabry pia akikwama kuhusu kuongezwa kwa mkataba.