Hongera!Nahodha wa Manchester United Harry Maguire amefunga pingu za maisha

Muhtasari
  • Nahodha wa Manchester United Harry Maguire amefunga pingu za maisha
Nahodha wa Manchester United Harry Maguire amefunga pingu za maisha
Image: HARRY MAGUIRE/INSTAGRAM

Nahodha wa Manchester United Harry Maguire amefunga pingu za maisha na mpenzi wake wa muda mrefu Fern Hawkins.

Wawili hao ambao wamekuwa pamoja kwa miaka 11, walifunga ndoa katika ukumbi wa Chateau de Varennes nchini Ufaransa siku ya Jumamosi.

Waliandamana na familia na marafiki.

Katika ujumbe wa kufurahisha moyo kwenye Instagram, nyota huyo  alishiriki picha ya kupendeza akimbusu mkewe, akiwa amevalia suti ya kijivu iliyomkaa huku Hawkins aking'aa katika gauni jeupe linalong'aa.

Aliandika, "Siku ambayo sitaisahau."

Wenzi hao walitangaza kuchumbiana kwao mnamo 2018 wakati wa safari ya kimapenzi kwenda Paris.

Mshabiki na marafiki walimpongeza mchezaji huyo kwa hatua yake mpya maishani.